BoT: Tunatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga uchumi wa nchi | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

BoT: Tunatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga uchumi wa nchi

BENKI Kuu Tanzania (BoT) imesema kuwa inatambua kazi inayofanywa na vyombo vya habari ya kutangaza habari mbalimbali za uchumi, fedha na biashara maeneo ambayo yanaigusa Benki Kuu na taifa kwa ujumla.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
25 Feb 2025
BoT: Tunatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga uchumi wa nchi

BENKI Kuu Tanzania (BoT) imesema kuwa inatambua kazi inayofanywa na vyombo vya habari ya kutangaza habari mbalimbali za uchumi, fedha na biashara maeneo ambayo yanaigusa Benki Kuu na taifa kwa ujumla.

Aidha BoT imewahimiza waandishi wa habari kuendelea kutumia nafasi waliyonayo kuchangia ujenzi wa uchumi wa nchi kwa ajili ya ustawi wa wananchi kwa ujumla.

Wito huo umetolewa leo Februari 25, 2025 mkoani Mtwara na Mkurugenzi wa BoT Tawi la Mtwara, Nassoro Omary wakati akifungua semina ya siku tatu kwa waandishi wa habari akimwakilisha Naibu Gavana wa BoT, Julian Banzi.

"Ni wazi kwamba Benki Kuu inatambulika, kazi zake zinajulikana na wananchi wanaijua kupitia kazi kubwa inayofanywa na vyombo vya habari katika kutangaza masuala mbalimbali yanayohusu taasisi hii ya umma. Pasipo habari zenu, makala zenu, na matangazo yenu, picha zenu na vipindi vyenu kuhusu Benki Kuu, inawezekana kabisa mafanikio ambayo Benki Kuu inajivunia kuwafikia wananchi walio wengi tusingekuwa nayo.

"Vyombo vya habari vinabakia kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu, kama ilivyo kwa sekta nyingi za kisiasa,Uchumi na kijamii. Kazi mnayoifanya katika kuhakikisha kwamba ajenda za maendeleo za taifa letu zinaeleweka na tunasonga mbele ni nzuri sana. Hongera sana waandishi wa habari kwa kazi hiyo njema mnayoifanya. Wito wangu ni kuwahimiza muendelee kutumia nafasi yenu adhimu kuchangia ujenzi wa uchumi wa nchi yetu kupitia taaluma yenu kwa ajili ya ustawi wa wananchi kwa ujumla," amesema.

Ameongeza kuwa BoT imenufaika kwa kazi inayofanywa na waandishi wa habari katika kutambua masuala yanayoendelea nchini na hata kuchukua hatua pale inapohitajika.

"Tunatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kuielimisha jamii kuhusu ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu za mikopo, hasa kwa huduma ndogo za fedha, ambako kumesababisha mateso na kero kubwa kwa wananchi. Kupitia taarifa hizo, Benki Kuu imeweza, kuchukua hatua mbalimbali kukomesha ukiukaji huo, na kuendelea  kutowa elimu endelevu ili kuhakikisha wananchi wanatambua namna bora ya kupata mikopo baada ya kuzingatia masuala yote muhimu. Aidha, ni kupitia vyombo vya habari taarifa mbalimbali zinawafikia wananchi kwa ujumla.

"Pia, dunia imekuwa inabadilika sana katika nyanja zote, kiuchumi, kisiasa, kijamii na hata maendeleo ya sayansi na teknolojia. Hivyo, ni wajibu wa Benki Kuu, kila inapowezekana kukutana na wadau kuwaelezea yanayoendelea duniani kwa lengo la kuhakikisha sote tunakwenda pamoja katika kutekeleza majukumu yetu bila ya wadau wengine kubakia nyuma. Kwa mfano, katika semina hii tutapata nafasi ya kujifunza mfumo mpya wa utekelezaji wa sera ya fedha ambao Benki Kuu ya Tanzania imeanza kuutekeleza kuanzia mwaka 2024," amesema na kuongeza:

"Bila mafunzo kama haya, itakuwa vigumu kwa sisi sote kwenda pamoja kuuelezea umma kuhusu sera ya fedha na hivyo inaweza kuwa sababu mojawapo ya utekelezaji kutokuwa rahisi kama tunavyotegemea," amesema.

Amefafanua kuwa katika semina hiyo, pamoja na mada kuhusu mfumo mpya wa sera ya fedha, pia kutakuwa na mada kuhusu umuhimu wa kutumia Shilingi ya Tanzania katika shughuli za uchumi hapa nchini, historia ya fedha za Tanzania, alama za usalaama na utunzanji wa fedha hizo, umuhimu wa kuwa na akiba ya dhahabu kama sehemu ya hifadhi ya taifa ya fedha za kigeni; utekelezaji wa Kanuni za Kumlinda Mteja wa huduma za kibenki na majukumu ya Benki Kuu kwa ujumla.

Akiwasilisha mada kuhusu Sera ya Fedha inayotumia Riba ya Benki Kuu, Mchumi kutoka Kurugenzi ya Uchumi, Sera na Utafiti wa BoT, Dominick Mwita amesema Sera ya Fedha ni msingi muhimu katika kufikia malengo ya kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

"Kutokana na changamoto zilizoambatana na mfumo wa sera ya fedha unaotumia ujazi wa fedha l, kuanzia Januari 2024, Benki Kuu imehamia katika mfumo mpya wa sera ya fedha unaolenga riba.

"Mfumo unaotumia riba ndio unaotumiwa na nchi duniani na una faida za ziada ukilinganisha na mfumo unaotumia ujazi wa fedha," amesema

Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.

Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.

UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.

UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.

KIWANGO Cha Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali Kimepanda Kutoka Shilingi Bilioni 624.61 hadi Bilioni 753.82

KIWANGO Cha Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali Kimepanda Kutoka Shilingi Bilioni 624.61 hadi Bilioni 753.82

JUMLA YA MIRADI 2,020 IMEFANIKIWA KUSAJILIWA NA TIC.

JUMLA YA MIRADI 2,020 IMEFANIKIWA KUSAJILIWA NA TIC.