KIWANGO Cha Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali Kimepanda Kutoka Shilingi Bilioni 624.61 hadi Bilioni 753.82 | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

KIWANGO Cha Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali Kimepanda Kutoka Shilingi Bilioni 624.61 hadi Bilioni 753.82

Kiwango cha makusanyo ya maduhuli ya Serikali kimepanda kutoka Shilingi bilioni 624.61 zilizokusanywa Mwaka wa Fedha 2021/2022 hadi kufikia Shilingi bilioni 753.82 Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
05 Mar 2025
KIWANGO Cha Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali Kimepanda Kutoka Shilingi Bilioni 624.61 hadi Bilioni 753.82

Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani M. Lwamo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa tume hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita tarehe 4 Machi, 2025, katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma.

Aidha amesema Makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la asilimia 20.7 ya makusanyo kwa miaka mitatu ambapo katika kipindi cha kuanzia Julai, 2024 hadi Februari, 2025, Tume imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 690,763,401,639.06 sawa na aslimia 69.08 ya lengo la Mwaka wa Fedha 2024/2025.

Aidha Mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 7.2 Mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 9.0 Mwaka 2023.

"Hii ni kutokana na kuimarika kwa usimamizi wa shughuli mbalimbali za Madini, ukuaji wa Sekta ya Madini umeongezeka kutoka asilimia 9.4 Mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 11.3 Mwaka 2023. Kutokana na kuendelea kuimarika kwa Sekta ya Madini, mwenendo wa Mchango wa Sekta ya Madini na ukuaji wake unatarajiwa kufikia asilimia 10 na zaidi ifikapo Mwaka 2025 kama ilivyoelezwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025"

Vile vile, katika kipindi kinachorejewa, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kwa kushirikiana na Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini iliendelea kusimamia utendaji kazi wa Masoko ya Madini na vituo vya ununuzi wa Madini nchini.

Aidha Hadi kufikia mwezi Februari, 2025 , Tume ya Madini kwa kushirikiana na TAMISEMI imefanikiwa kuanzisha masoko 43 na vituo vya ununuzi 109,kuanzia Mwaka wa Fedha 2021/2022 mauzo ya madini katika Masoko na Vituo vya Ununuzi wa madini yameendelea kuongezeka kutoka Shilingi 2,361.80 bilioni hadi Shilingi 2,597.18 bilioni kwa Mwaka 2023/2024.

"Mauzo hayo yamesababisha Tume ya Madini kukusanya maduhuli ya Serikali. Maduhuli hayo yanatokana na Mrabaha na Ada ya Ukaguzi wa madini yaliyouzwa kwenye Masoko na Vituo vya Ununuzi wa madini"

Sanjari na hayo Tume ya Madini katika kuhakikisha kuwa Wananchi wananufaika na rasilimali madini, imeendelea kusimamia uwasilishaji wa Mipango ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini (LCPs) kutoka kwa Wamiliki na Waombaji wa leseni za madini, wasambaza bidhaa na watoa huduma kama takwa mojawapo la Sheria ya Madini Sura ya 123.

"Katika kipindi rejewa, jumla ya Mipango 1,076 ya Ushirikishwaji wa Tanzania katika Sekta ya Madini ilipokelewa na kufanyiwa uchambuzi. Kati ya Mipango iliyowasilishwa, 1,047 ilikidhi vigezo na kuidhinishwa na Mipango 29 haikukidhi vigezo hivyo ilirejeshwa kwa wahusika kwa ajili ya marekebisho"

Aidha Tume ya Madini imeendelea kusimamia kikamilifu upatikanaji wa Ajira kwa Watanzania kutoka kwenye Kampuni mbalimbali za uchimbaji ambapo katika kipindi rejewa Kampuni ziliweza kuzalisha ajira   19,874 ambapo kati ya hizo 19,371 ni Watanzania   sawa na asilimia 97.5 na 503 ni wageni sawa asilimia 2.5 ya ajira zote zilizozalishwa. Vilevile, Jumla ya bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani (USD) 3,780,161,183.28 ziliuzwa na kusambazwa migodini ambapo kati ya bidhaa hizo Kampuni za Watanzania zilifanikiwa kuuza bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani (USD) 3,465,592,451.28 sawa asilimia 91.68 ya thamani ya mauzo ya bidhaa zote na huduma zilizotolewa migodini.

Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.

Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.

UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.

UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.

JUMLA YA MIRADI 2,020 IMEFANIKIWA KUSAJILIWA NA TIC.

JUMLA YA MIRADI 2,020 IMEFANIKIWA KUSAJILIWA NA TIC.

BoT: Tunatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga uchumi wa nchi

BoT: Tunatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga uchumi wa nchi