

Benki Kuu Tanzania imesema hadi sasa ina akiba ya dhahabu fedha zaidi ya tani mbili huku lengo likiwa kufikia tani sita kwa mwaka.
Benki Kuu Tanzania imesema hadi sasa ina akiba ya dhahabu fedha zaidi ya tani mbili huku lengo likiwa kufikia tani sita kwa mwaka.
Hayo yameelezwa leo Februari 25, 2024 na Mchambuzi wa Masoko ya Fedha kutoka BoT, Dunga Nginila wakati akiwasilisha mada ya Umuhimu wa Benki Kuu kuwa na dhahabu kama sehemu ya akiba yake ya fedha za kigeni, kwenye semina kwa waandishi wa habari.
Amesema wameanza kununua dhahabu kutoka Tanzania tangu Oktoba mwaka jana ambapo lengo ni kufikisha tani sita kabla ya mwaka wa fedha kuisha.
"Dhahabu ina faida kubwa kweye nchi kama yetu ambayo tuna dhahabu nyingi. Kwahiyo faida kubwa tunaongeza akiba fedha za kigeni za nchi. na dhahabu fedha tunapoinunua na kuifikisha kwa wateja wetu inakuwa inahesabika kama fedha za kigeni za nchi," amesema.
Amefafanua kuwa, BoT inanunua dhahabu killa siku na wananunua dhahabu kutoka Tanzania tu kwani bado kuna akiba nyingi ya dhahabu.
DKT. BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA CLIMATE INVESTMENT FUNDS
KAMATI ya Bunge ya miundombinu yaridhishwa na kasi ujenzi daraja la pangani
MIKOA 16 kunufaika na Nishati ya Jotoardhi
MASAA YA Upatikanaji wa Huduma ya Maji Yameongezeka Kutoka saa 16 hadi saa 22
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wadau wa kemikali
Hatua Kali Za Kisheria Kuchukuliwa Kwa Watakaoghushi Cheti Cha Kuhitimu Mafunzo ya JKT.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.