

Ajira za moja kwa moja katika Sekta ya Utalii zimeongezeka ambapo zaidi ya watu 856 wameajiriwa na zaidi ya watu 1,120 wanajihusisha na shughuli za usafirishaji, uongozaji na malazi ya watalii
Kuongezeka kwa kiwango cha uzalishaji wa mazao ya misitu na nyuki kutoka asilimia 23 hadi asilimia 71 pamoja na Kuongezeka kwa vikundi vya wazalishaji wa mazao ya misitu na nyuki kutoka vikundi 86 hadi vikundi 243
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Batilda Buriani wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita tarehe 15 Julai 2025 katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.
Aidha amesema kuwa Kuongezeka kwa maeneo ya ufugaji wa nyuki kutoka 12 hadi 19,Kuongezeka kwa misitu iliyohifadhiwa kwa ajili ya biashara ya kaboni kutoka 0 hadi 3,naKuongezeka kwa miti iliyopandwa kutoka miti 8,142,122 hadi miti 11,902,125
Aidha Mradi wa Maboresho ya Bandari ya Tanga Katika kipindi cha mwaka 2020 hadi Aprili 2025, kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) umetekeleza mradi mkubwa wa kimkakati wa maboresho ya Bandari ya Tanga kwa awamu mbili yenye thamani ya shilingi bilioni 429.1.
Mafanikio Baada ya Maboresho Kukamilika ni pamoja na Ufanisi umeongezeka katika kuhudumia meli na shehena ambapo muda wa kuhudumia meli umepungua kutoka siku 5 hadi siku 2,Ongezeko la meli 198 mwaka 2021 hadi meli 307 mwaka 2025 na shehena kutoka tani 888,130 mwaka 2021 hadi tani 1,191,480 zinazopakuliwa na kupakiliwa na makasha TEUS 7,036 hadi makasha 7,817 katika Bandari ya Tanga,Mapato yameongezeka pamoja na ajira za muda mrefu na muda mfupi.
Aidha, Mkoa umepokea kiasi cha thamani ya shilingi 1,118,092,480.00 kwajili ya Ukarabati mkubwa wa kivuko cha MV Tanga ili kusaidia wananchi kupata huduma hiyo kwa urahisi zaidi.
"Mkoa unaendelea kutekeleza misingi ya Utawala bora kwa Kutenga siku ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi kwa wakati, taarifa ya utatuzi wa kero za wananchi huratibiwa na Mkoa na kuwasilishwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI kila mwezi,Kila Taasisi imeunda Kamati ya Kudhibiti Uadilifu kwa watumishi wake ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa wananchi bila upendeleo wala ubaguzi wa aina yoyote,TAKUKURU inaendelea na jukumu lake la Kuzuia na Kupambana na Vitendo vyote vya rushwa kwenye Taasisi za Umma na binafsi"
"TAKUKURU wameendelea na kazi ya kuokoa mali na rasilimali za Umma ambazo zilikuwa zinaelekea kupotea kupitia watumishi wasio waaminifu,Kwa kipindi cha mwaka 2020 Mkoa ulikuwa na mahakama za mwanzo 65 na wilaya 6 hadi kufikia mwaka 2025 Mkoa una mahakama za mwanzo 67 na Wilaya 8 hii inaonyesha kuna ongezeko la mahakama za mwanzo 2 na wilaya 2,Ujenzi wa majengo ya ofisi za wakurugenzi na nyumba za viongozi, Mkoa umepokea fedha kwajili ya ujenzi wa Majengo ya Utawala,Samani za Ofisi, Nyumba za wakurugenzi na Wakuu wa Idara"Amesisitiza Mhe.Buriani
Kwa upande wa Sekta ya Elimu katika Mkoa wa Tanga inajumuisha Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu,kupitia fedha za ujenzi wa miundombinu zilizotolewa na Serikali, mafanikio mengi yamepatikana katika sekta ya Elimu ikiwemo ongezeko la ufaulu, idadi ya Shule pamoja na miundombinu ya shule ikiwemo,Ujenzi wa shule mpya, vyumba vya madarasa,nyumba za walimu, mabweni, mabwalo ambavyo vimerahisisha shughuli za ufundishaji wa wanafunzi katika shule za Msingi na Sekondari.
Hali ya Utekelezaji wa Bomba la Mafuta kwa sasa ni Fidia kwa wananchi waliopisha Mkuza wa Bomba Mkoa wa Tanga imefikia 98.7% ambapo kati ya wananchi 1580, wananchi 1560 wameshapokea malipo ya fidia jumla Shilingi billion 9.38, Aidha Wananchi 40 wamejengewa nyumba 43 za makazi mbadala ambazo ujenzi wake umekamilika kwa 100% na kukabidhiwa kwa wahusika.
Wananchi wamepata ajira kwenye maeneo yote mradi ulipopita, kwa eneo la Chongoleani pekee kuna ajira 810,Biashara za huduma kama vile Mama/baba lishe,Kuongezeka kwa mzunguko wa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii, na huduma ndogo za kifedha.
Kwa mujibu wa takwimu za matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, 2022 Mkoa wa Tanga una idadi ya watu 2,615,597 (wanaume 1,275,665 na wanawake 1,339,932) na Ongezeko la watu kwa mwaka ni asilimia 2.5.Inayopelekwea idadi ya watu kufikia 2,861,741 kwa mwaka 2025 (wanaume 1,406,476 na wanawake 1,455,265)
Hali ya ulinzi na usalama ni shwari. Vyombo vya dola vimeendelea kufanya doria za mara kwa mara ili kuimarisha usalama wa ndani na mipaka ya nchi kavu pamoja na baharini. Katika kipindi hiki hakuna matukio makubwa yaliyojitokeza yenye kuhatarisha usalama wa Mkoa.
Kwa mujibu wa Takwimu wa NBS kwa mwaka 2024, pato la Mkoa (GDP) limeongezeka kutoka wastani wa shilingi Trilioni 6.818 kwa mwaka 2020 hadi shilingi Trilioni 9.581 kwa mwaka, 2024 sawa na asilimia 4.7 ya Pato la Taifa ambalo ni shilingi Trilioni 205.846.
Aidha, wastani wa pato la Mtu mmoja (Per Capital Income) limeongezeka kutoka wastani wa shilingi milioni 2.783,908.00 kwa mwaka 2020 hadi shilingi milioni 3,433,368.00 kwa mwaka, 2024. Ikiwa ni juu ya wastani wa kitaifa wa shilingi 3,204,244.00. Takwimu hizi zinauweka Mkoa wa Tanga kushika nafasi ya sita (6) kati ya Mikoa yote ya Tanzania Bara katika vita dhidi ya umaskini pamoja na mchango wa pato la Taifa.
Shughuli za kiuchumi na uzalishaji zinazotekelezwa na Wananchi wa Mkoa wa Tanga zipo kwenye maeneo mbalimbali zikiwemo Sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Maliasili na Utalii. Aidha, Shughuli nyingine za uzalishaji zinatokana na ukuaji wa Sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji unaozingatia ujasiriamali katika sekta za umma na binafsi. Hata hivyo, Wananchi walio wengi zaidi ya asilimia 80 wamejikita katika shughuli za Kilimo, mifugo na uvuvi, asilimia tisa (9) wanajishughulisha na shughuli za mazao ya misitu, ufugaji nyuki na uchimbaji madini, asilimia sita (6) wanajishughulisha na shughuli za biashara, uendeshaji wa viwanda,usafirishaji na uchukuzi na Sekta ya Fedha. Halikadhalika asilimia tano (5) wameajiriwa katika sekta za umma na binafsi kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
Simiyu Yajivunia Ongezeko La Mapato TRA kutoka Bilioni 9.55 Hadi Bilioni 25.46
Mkoa Wa Mara Umezalisha Dhahabu Yenye Uzito Wa Tani 58.90 Sawa na Trillioni 6.90
WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSOMA KATIBA, SHERIA, KANUNI ZA TUME
SALALI:Tunampongeza Rais Samia Kwa Kujumuisha Watu Wenye Ulemavu Dira 2050.
Rais Samia Azindua Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050, Asisitiza Utekelezaji Wa Vitendo Na Upimaji Wa Matokeo
IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.
Uzalishaji wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 7.9 Hadi Tani 42.5
DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.
WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI.
WATENDAJI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 WAFUNDWA