SALALI:Tunampongeza Rais Samia Kwa Kujumuisha Watu Wenye Ulemavu Dira 2050. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

SALALI:Tunampongeza Rais Samia Kwa Kujumuisha Watu Wenye Ulemavu Dira 2050.

Mkurugenzi Mtendaji waTaasisi ya Foundation For Disabilities Hope (FDH) Maiko Salali amempongeza Rais Samia Kwa kuweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Kwa kuwajumuisha watu wenye ulemavu.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
17 Jul 2025
SALALI:Tunampongeza Rais Samia Kwa Kujumuisha Watu Wenye Ulemavu Dira 2050.

Ametoa kauli hiyo jijini Dodoma mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuzindua rasmi dira hiyo leo Julai 17, 2025.

Salali amesema FDH inatambua na kupongeza namna mchakato wa maandalizi ya Dira hiyo ulivyokuwa shirikishi, ukihusisha mawazo ya makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu.

Ameeleza kuwa dira hiyo inakwenda kujibu changamoto nyingi ambazo watu wenye ulemavu wamekuwa wakikumbana nazo kwa miaka mingi, zikiwemo ukosefu wa fursa za kiuchumi, miundombinu isiyo rafiki, upatikanaji hafifu wa elimu jumuishi na huduma duni za afya.

“Kwetu sisi wenye ulemavu, hii dira ina maana kubwa kwa kuwa inaweka mwelekeo wa wazi wa kutatua changamoto zetu kupitia sera na mifumo jumuishi,tunatoa wito kwa watu wote wenye ulemavu kuisoma, kuielewa na kufuatilia utekelezaji wake,” amesema Salali.

Aidha, Salali amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa moyo wake wa kuwatambua na kuwawezesha watu wenye ulemavu, akitaja mafanikio kadhaa ya Serikali ya Awamu ya Sita ikiwemo kuimarishwa kwa elimu jumuishi, uwepo wa Sera na Dira mahsusi ya watu wenye ulemavu, ajira serikalini, vifaa saidizi na ushirikishwaji kwenye mabaraza ya maamuzi.

" Haya ni matokeo ya dhamira ya kweli ya Rais kuhakikisha hakuna Mtanzania anayebaki nyuma katika safari ya maendeleo, "amesema Mkurugenzi huyo wa FDH

Amesema kuwa msingi wa maendeleo ya taifa lolote hujengwa kwenye kupanga kwa weledi, na kueleza kuwa dira hii inawakilisha maono ya pamoja kuhusu Tanzania ya baadaye.

“Kila hatua ya maendeleo huanzia kwenye kupanga,na ni lazima tukubaliane, sisi Watanzania tunatazama zaidi namna mpango huu unavyotekelezwa kwa ufanisi,”

DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.

DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.

DKT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA TANZANIA NATIONAL COORDINATING MECHANISM (TNCM)

DKT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA TANZANIA NATIONAL COORDINATING MECHANISM (TNCM)

DCEA YABAINI NJIA MPYA INAYOTUMIWA NA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA  KUSAFIRISHIA DAWA HIZO.

DCEA YABAINI NJIA MPYA INAYOTUMIWA NA WAFANYABIASHARA WA DAWA ZA KULEVYA KUSAFIRISHIA DAWA HIZO.

CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA

CPA KASORE ASISITIZA UMUHIMU WA KUFUNDISHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KWA WATOTO ILI WAWEZE KUJITEGEMEA

TPDC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAPATA TUZO SABASABA.

TPDC YAJIVUNIA MAFANIKIO YAPATA TUZO SABASABA.