

Ufugaji wa samaki kwa kutumia njia ya kisasa umeongezeka kutoka vizimba (fish cauges) 1,664 mwaka 2020 hadi 2,715 mwaka 2025 sawa na ongezeko la vizimba 1,051.
Jumla ya tani 43,657.6 za minofu ya Samaki zimechakatwa na tani 81,812 zimesafirishwa kwenda soko la nje ya Nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa kipindi cha mwaka 2024
Akizungumza Julai 16 2025 na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amesema Kilo za mabondo zilizosafirishwa kwenda soko la nje ya Nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwanza zimeongezeka kutoka kilo 431,721 mwaka 2020 hadi kilo 495,448 mwaka 2024 sawa na ongezeko la kilo 63,727.
Aidha Idadi ya mabwawa ya ufugaji wa Samaki imeongezeka kutoka 286 mwaka 2020 hadi mabwawa 531 mwaka 2025 sawa na ongezeko la mabwawa 245.
Aidha Kiasi cha mapato yaliyotokana na shughuli za uvuvi kimeongezeka kutoka Shilingi 4,416,172,821.59 mwaka 2020 hadi Shilingi 8,233,724,351.33 mwaka 2025 sawa na ongezeko la Shilingi 3,817,551,529.74.
“Haya mafanikio ni ushahidi kuwa juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha uchumi wa buluu na sekta ya uvuvi zimezaa matunda Mapato kutokana na shughuli za uvuvi yameongezeka kutoka shilingi bilioni 4.4 mwaka 2020 hadi bilioni 8.2 mwaka 2025,” amesema Mtanda.
Amesisitiza kuwa mkoa utaendelea kuhamasisha uwekezaji, utafiti na matumizi ya teknolojia ili kuhakikisha wananchi wa Mwanza, wakiwemo wavuvi wadogo na wafanyabiashara wa dagaa, wananufaika ipasavyo na rasilimali za Ziwa Victoria.
Aidha kwenye Sekta ya Elimu Miundombinu imeboreshwa ambayo imesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa umbali wa kutembea kwenda shule, msongamano wa wanafunzi madarasani, kuwezesha mazingira bora zaidi kwa walimu na wanafunzi.
Aidha jumla ya Shilingi Trilioni 5.6 zimepokelewa Mkoani kipindi cha mwezi Novemba, 2020 hadi Aprili, 2025 kwa ajili ya maendeleo ya sekta mbalimbali.
"Jumla ya Shilingi Bilioni 63.2 zimetolewa, Mafanikio makubwa katika Sekta ya Afya ni wananchi kupata huduma kirahisi, kupunguza kusafirisha wagonjwa kwenda nje kwa kuendelea kupata huduma za kibingwa ambazo ni huduma za kibigwa za upasuaji, huduma za kibingwa za mifupa, huduma za kibingwa za afya ya uzazi, huduma za kibingwa za sikio, pua na kinywa, huduma za kibingwa za magonjwa ya ndani pamoja huduma za kibingwa za saratani na huduma za kibingwa za magonjwa ya dharura"Amesisitiza Mtanda
Aidha Kuanzia Julai 2020 hadi Mei 2025, imekamilisha jumla ya miradi 80 yenye thamani ya Shilingi 100,338,450,084.06 ambayo imepelekea hali ya upatikanaji wa maji vijijini kuimarika kwa kiwango kikubwa kutoka 57% 2021 hadi 77% mwaka 2025 kwa mchanganuo ufuatao:- Wilaya ya Kwimba imepanda kutoka 58% hadi 77.3%, Magu kutoka 44% hadi 73%, Misungwi kutoka 70.4% hadi 77.3%, Sengerema 57% hadi 91% na Ukerewe 56% hadi 91%.
Sanjari na hayo Jumla ya Shilingi 18,674,414,228.51 zimetolewa Mradi wa ujenzi wa vivuko vipya vitano (5) vya Kisorya – Rugenzi Wilaya ya Ukerewe - chenye thamani ya Shilingi 892,760,706.00 Ijinga – Kahangala 5,255,080,099.51 – Magu, Bwiro – Bukondo Shilingi 676,164,840.00 - Ukerewe Nyakarilo – Kome Shilingi 8,033,344,250.00 - Buchosa, Buyagu - Mbalika Shilingi 3,817,064,333.00 unaendelea.- Misungwi. Vivuko 12 vilivyopo vimeendelea kufanyiwa ukarabati ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Aidha jumla ya Shilingi Bilioni 85.8 zimewezesha Wananchi KiuchumiVikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu vilivyopewa mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba vimeongezeka kutoka 630 hadi 1,856, kiwango cha mikopo iliyotolewa nacho kimeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 3.3 hadi Shilingi. Bilioni 14.1.
Kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF), Jumla ya kaya 59,932 zimenufaika Shilingi Bilioni 44 zimetolewa kwa walengwa.
Aidha Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 640,205.3 (37.59%) 2020/21 hadi kufikia tani 1,025,784.08 (60.23%) mwaka 2024/25 sawa na ongezeko la Tani 385,578 (22.64%)
"Ujenzi na ukarabati wa miradi ya umwagiliaji 2 ya Sengerema Katunguru na Mahiga kwimba kwa gharama ya Shilingi. 54,473,623,973.41 unaendelea Upatikanaji wa viuatilifu umeongezeka kutoka chupa 324,821 Mwaka 2020 hadi chupa 832499 Mwaka 2025"
Simiyu Yajivunia Ongezeko La Mapato TRA kutoka Bilioni 9.55 Hadi Bilioni 25.46
Mkoa Wa Mara Umezalisha Dhahabu Yenye Uzito Wa Tani 58.90 Sawa na Trillioni 6.90
WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSOMA KATIBA, SHERIA, KANUNI ZA TUME
SALALI:Tunampongeza Rais Samia Kwa Kujumuisha Watu Wenye Ulemavu Dira 2050.
Rais Samia Azindua Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050, Asisitiza Utekelezaji Wa Vitendo Na Upimaji Wa Matokeo
IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.
AJIRA ZA MOJA KWA MOJA KATIKA SEKTA YA UTALII ZIMEONGEZEKA.
Uzalishaji wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 7.9 Hadi Tani 42.5
DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.
WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI.