

Mkoa wa Mara umezalisha dhahabu yenye uzito wa tani 58.90 ikiwa na thamani ya shilingi trilioni 6.90 kutoka kwa wachimbaji wakubwa, wakati na wadogo.
Katika kipindi hicho Serikali imekusanya maduhuli ya shilingi bilioni 568 kutokana na malipo ya mrahaba, ada ya ukaguzi kwenye mauzo ya madini, ada za leseni na tozo mbalimbali za vibali, ushuru wa huduma katika Halmashauri na kodi ya zuio inayokatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.KANALI EVANS ALFRED MTAMBI wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita tarehe 18 Julai katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.
Aidha katika Sekta ya Madini kuna urudishwaji wa faida kwa jamii kutoka kwa wamiliki wa leseni na kampuni za uchimbaji madini (CSR). Kwa miaka hii minne kumekuwa na utekelezaji wa miradi 398 ya huduma za jamii yenye thamani ya shilingi bilioni 33.81 zitokanazo na CSR ya sekta ya madini.
"Katika kipindi hiki Serikali imeboresha majengo ya utawala kwa ajili ya kuboresha mazingira ya utoaji huduma kwa wananchi. Majengo yaliyojengwa ni Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama, majengo ya utawala ya Halmashauri sita yamekamilika na ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti umeanza katika mwaka wa fedha 2025/2026 na unaendelea"
Aidha, Serikali imenunua magari ya viongozi ikiwa ni pamoja na gari la Mkuu wa Mkoa, magari ya Wakuu wa Wilaya zote sita na magari kwa ajili ya Idara na Vitengo vya Sekretarieti ya Mkoa wa Mara.
"Katika kipindi hiki, majengo ya ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Butiama, Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Butiama yamejengwa"
Aidha, Serikali imejenga jengo la Mahakama Kuu Musoma, nyumba 02 za Majaji na mahakama mbili za Wilaya katika Wilaya za Butiama na Rorya.
"Ujenzi wa majengo haya ya utawala umeboresha mazingira ya kutolea huduma kwa wananchi, mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi na mandhari ya maeneo hayo"
Sanjari na hayo Mkoa wa Mara ni kati ya mikoa yenye utajiri mkubwa wa madini ikiwemo dhahabu, fedha, shaba, chuma, madini ya ujenzi, madini ya viwandani na madini ya vito. Madini ya dhahabu ndio yanayochimbwa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na madini mengine.
Hadi kufikia Juni, 2025 Mkoa ulikuwa na lesseni 2,288 ambazo zinahusisha uchimbaji wa madini, utafiti, uchenjuaji na biashara ya madini.
Aidha, Mkoa kwa kushirikiana na Tume ya Madini na Mgodi wa Barrick North Mara umewawezesha upatikanaji wa lesseni 104 kwa vikundi 48 vyenye jumla ya Vijana 1,836 kutoka vijiji 13 katika eneo la Nyamongo, Wilaya ya Tarime.
"Uwezeshaji wa makundi hayo ni semehu ya utekelezaji wa programu ya Mining for a Brighter Tomorrow (MBT) na una lengo la kutoa fursa kwa vijana kushiriki katika mnyororo wa thamani wa madini"
"Vijana hao wanapatiwa elimu kuhusu uchimbaji wa madini chini ya uangalizi wa Mgodi wa Barrick North Mara, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Ofisi ya Madini Mkoa"Amesisitiza
Serikali imetoa miongozo ya kuyawezesha makundi mbalimbali katika jamii kuweza kuimarisha uwezo wao wa kushiriki shughuli za maendeleo na kuleta usawa wa kiuchumi katika jamii.
"Katika kipindi hiki, kuna ongezeko la vikundi vinavyonufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri za Mkoa wa Mara kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kutoka vikundi 187 mwezi Novemba, 2020 hadi vikundi 324 Aprili, 2025"
Aidha, fedha zinazotolewa kama mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulamavu zimeongezeka kutoka shilingi bilioni 1.63 Novemba 2020 hadi shilingi bilioni 5.88 mwaka 2025.
Aidha, kumekuwa na ongezeko la vikundi vya wanawake kutoka vikundi 92 Novemba, 2020 hadi 99 Aprili, 2025; vikundi vya vijana kutoka 53 hadi 139 na vikundi vya watu wenye ulemavu kutoka 42 hadi 86. Mafanikio yaliyopatikana kutokana na vikundi hivi ni pamoja na kuongezeka kwa ajira, uchumi wa vikundi, mtu mmoja mmoja na kupunguza utegemezi wa makundi hayo katika jamii.
Mkoa wa Mara unatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) ambapo kwa sasa Mkoa una jumla ya wanufaika 50,934 hadi kufikia Juni, 2025. Kutokana na mpango huu wananchi kutoka kaya maskini wameweza kuboresha maisha yao kwa kujifunza na kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.
Simiyu Yajivunia Ongezeko La Mapato TRA kutoka Bilioni 9.55 Hadi Bilioni 25.46
WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSOMA KATIBA, SHERIA, KANUNI ZA TUME
SALALI:Tunampongeza Rais Samia Kwa Kujumuisha Watu Wenye Ulemavu Dira 2050.
Rais Samia Azindua Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050, Asisitiza Utekelezaji Wa Vitendo Na Upimaji Wa Matokeo
UFUGAJI WA SAMAKI KWA KUTUMIA NJIA YA KISASA UMEONGEZEKA.
IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.
AJIRA ZA MOJA KWA MOJA KATIKA SEKTA YA UTALII ZIMEONGEZEKA.
Uzalishaji wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 7.9 Hadi Tani 42.5
DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.
WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI.