Uzalishaji wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 7.9 Hadi Tani 42.5 | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

Uzalishaji wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 7.9 Hadi Tani 42.5

Uzalishaji wa madini umeongezeka kutoka tani 7.9 Kwa mwaka 2020 hadi tani 42.5 mwaka 2025 ambapo ongezeka la fedha za kigeni zilizotokana na uuzaji wa madini kutoka Dola za Marekani milioni 44.33 mwaka 2020 hadi Dola za Marekani milioni 191.15 mwaka 2025

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
14 Jul 2025
Uzalishaji wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 7.9 Hadi Tani 42.5

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Mboni Mohamed Mhita wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita tarehe 14 Julai 2025 katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma.

Aidha Kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri yatokanayo na 
uchimbaji wa madini ni  kutoka Shilingi milioni 745.4 mwaka 2020 
hadi Shilingi 3,334,265,389.56 mwaka 2025 pamoja na Kuongezeka kwa masoko na vituo vya ununuzi madini kutoka 06 mwaka 2020 hadi vituo 12 mwaka 2025.

"Kuongezeka kwa utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo kutoka 
leseni 332 mwaka 2020 hadi 1,766 mwaka 2025,Kuongezeka kwa makusanyo ya maduhuli kutoka shilingi bilioni 
103.4 mwaka 2020/21hadi kufikia shilingi bilioni 607.04 mwaka 2024/25, Kuanzisha masoko ya madini katika maeneo ya Wilaya za 
Kahama na Shinyanga"

Aidha Mkoa wa Shinyanga umepokea 
Shilingi trilioni 1.563 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo 
katika sekta za afya, elimu, miundombinu ya usafiri na usafirishaji, maji, nishati, madini, kilimo, mifugo, viwanda, biashara, uwezeshaji wananchi kiuchumi na miradi ya kimkakati.

Sanjari na hayo  Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya mifugo, hatua ambayo imechangia kuongezeka kwa tija na kipato kwa wafugaji wa mkoa huo.

Aidha amesema kuwa mkoa umeona mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitano, ikiwa ni matokeo ya mikakati ya kitaifa ya kuendeleza sekta ya mifugo, uwekezaji katika huduma za ugani na elimu kwa wafugaji.

Amesema uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita 10,031,225 mwaka 2020 hadi lita 18,335,300 mwaka 2025, huku uzalishaji wa nyama ukipanda kutoka tani 3,150 hadi tani 5,600 katika kipindi hicho.

Aidha, uzalishaji wa ngozi nao umeongezeka kutoka vipande 58,035 mwaka 2020 hadi vipande 108,770 mwaka 2025, hali inayoonyesha uboreshaji wa thamani ya mifugo inayofugwa mkoani humo.

Katika kuongeza ufanisi wa huduma za mifugo, Mhita amesema serikali imesambaza lita 2,060.5 za dawa za kuogeshea mifugo, pamoja na dozi 823,000 za chanjo kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa wa sotoka ya mbuzi na kondoo.

Mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa majosho 16 mapya yamejengwa katika Halmashauri za Kishapu, Shinyanga DC, Shinyanga MC na Ushetu, ili kurahisisha huduma ya kuogesha mifugo kwa lengo la kuzuia magonjwa ya ngozi na kuimarisha afya ya mifugo.

Katika kuboresha huduma za ugani, serikali imesambaza pikipiki 54 kwa maafisa mifugo, hatua iliyosaidia kufikisha elimu ya ufugaji bora kwa wafugaji wa vijijini. Pia, mashamba darasa manne ya malisho ya mifugo yameanzishwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wafugaji kutumia malisho bora.

Mhe. Mhita amesema pia kuwa elimu juu ya ufugaji wa kisasa na uboreshaji wa mbari za mifugo imetolewa kwa wafugaji wengi, huku serikali ikisambaza mbegu bora za mifugo kupitia njia ya uhimilishaji, zikiwemo aina za Bosmara, Aryshire na Frisian.

Amesisitiza kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha maisha ya wananchi kupitia sekta za uzalishaji, hasa kwa jamii za wafugaji

"Shinyanga ni miongoni mwa mikoa inayotegemea mifugo kwa kiasi kikubwa. Serikali ya Awamu ya Sita imeweka nguvu kubwa katika kuhakikisha wafugaji wananufaika moja kwa moja na shughuli zao. Tunaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mipango yote ya maendeleo ya sekta hii,” amesema Mhe. Mhita.

Mkuu huyo wa mkoa ameahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa mifugo inatumika kama chanzo kikuu cha kipato, chakula, ajira na maendeleo ya uchumi wa mkoa.
 

MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABA*

MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU SABASABA*

eGA Yaonesha Namna Serikali Inavyotekeleza Mageuzi Kidigitali kwenye Maonesho ya sabasaba.

eGA Yaonesha Namna Serikali Inavyotekeleza Mageuzi Kidigitali kwenye Maonesho ya sabasaba.

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA NISHATI MAONESHO YA SABASABA

BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA  KWA WATANZANIA.

BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.

DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.

DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.