

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa leo tarehe 13 Julai, 2025 amemkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati, Bi Neema Chalila Mbuja tuzo ya umahiri kufuatia mchango wake alioutoa wakati wa Maonesho ya Dunia ya Biashara ya Osaka nchini Japan kwa upande wa Mawasiliano na kuitangaza nchi.
*Ni kufuatia Umahiri wa masuala ya Mawasiliano kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025*
*Ampongeza kwa kuwa Kiongozi wa mfano wakati wa Mkutano wa Biashara na Uwekezaji na Utalii Osaka Expo 2025*
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa leo tarehe 13 Julai, 2025 amemkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati, Bi Neema Chalila Mbuja tuzo ya umahiri kufuatia mchango wake alioutoa wakati wa Maonesho ya Dunia ya Biashara ya Osaka nchini Japan kwa upande wa Mawasiliano na kuitangaza nchi.
Mhe Majaliwa amempongeza Bi. Mbuja wakati wa kilele cha Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba 2025.
Sambamba na hilo Mhe Majaliwa amempongeza Bi. Mbuja kwa kuwa muongozaji wa shughuli na kuwa mahiri wakati wa Kongamano la Kimataifa la Biashara, Uwekezaji na Utalii kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025.
Kwa upande wake Bi. Mbuja amemshukuru Mhe. Majaliwa kwa kukabidhi tuzo hiyo iliyotolewa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara TANTRADE na kuahidi kuendelea kuitangaza Wizara ya Nishati Kimataifa.
Simiyu Yajivunia Ongezeko La Mapato TRA kutoka Bilioni 9.55 Hadi Bilioni 25.46
Mkoa Wa Mara Umezalisha Dhahabu Yenye Uzito Wa Tani 58.90 Sawa na Trillioni 6.90
WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSOMA KATIBA, SHERIA, KANUNI ZA TUME
SALALI:Tunampongeza Rais Samia Kwa Kujumuisha Watu Wenye Ulemavu Dira 2050.
Rais Samia Azindua Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050, Asisitiza Utekelezaji Wa Vitendo Na Upimaji Wa Matokeo
IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.
AJIRA ZA MOJA KWA MOJA KATIKA SEKTA YA UTALII ZIMEONGEZEKA.
Uzalishaji wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 7.9 Hadi Tani 42.5
DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.
WATENDAJI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 WAFUNDWA