

CHAMA cha wanawake wachimbaji madini nchini (TAWOMA) kimetoa fursa kwa vijana wanaohitaji kujishughulisha katika uchimbaji kuweza kujifunza na kujitengenezea ajira ili kuongeza kipato chao binafsi na kuchangia katima pato la Taifa.
CHAMA cha wanawake wachimbaji madini nchini (TAWOMA) kimetoa fursa kwa vijana wanaohitaji kujishughulisha katika uchimbaji kuweza kujifunza na kujitengenezea ajira ili kuongeza kipato chao binafsi na kuchangia katima pato la Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuhitimishwa kwa maonesho ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba Katibu Mkuu wa TAWOMA Salma Ernest amesema wameanzisha programu ya vijana ili kuwasaidia kujiajiri kupitia sekta ya madini.
"Mpaka sasa kupitia program hiyo vijana zaidi ya 60 wamepata mafunzo kupitia sekta ya madini pamoja na wale waliomaliza kusoma chuo cha uchakataji madini kilichopo mkoani Arusha",Amesema.
Aidha ameongeza kuwa wanavijana ambao mamemaliza chuo cha madini cha Arusha ambapo wao ni wabunifu na wamepitia kujifunza uongezaji thamani madini ya vito ikiwa ni pamoja na kutengeneza vitu mbalimbali kama picha,na bidhaa mbalimbali za kuvaa wanawake na wanaume.
"Vijana hao wameongeza ujuzi wa kukata madini katika maumbo mbalimbali ambapo sasa wanauza kupitia duka ambalo lipo mtaa wa undali jijini Dar es salaam na bidhaa hapo zinapatikna kwa bei nafuu",amesema.
Kwa upande wake STANLEY EDward kutoka kituo cha jiolojia amesema watanzania wengi hawajui aina za madini mbalimbali yaliyopo nchini na fursa zitokanazo na madini hayo.
"Watanzania wengi hawajui aina za madini yaliyopo hapa nchini wengi wamezoea madini kama Tanzanite,dhahabu,silver,almasi,rubi,diamond lakini ukweli ni kwamba kuna madini mengi nchini na yanatoa fursa kwa vijana kuweza kujiajili",amesema.
Ameongeza kuwa kituo chao cha jiolojia kimekuwa kikitoa mafunzo kwenye uongezaji thamani kama ukataji na ung'arishaji wa bidhaa tofauti zinazotokana na madini hivyo ametoa rai kwa vijana kuchangamkia fursa hizo.
Simiyu Yajivunia Ongezeko La Mapato TRA kutoka Bilioni 9.55 Hadi Bilioni 25.46
Mkoa Wa Mara Umezalisha Dhahabu Yenye Uzito Wa Tani 58.90 Sawa na Trillioni 6.90
WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSOMA KATIBA, SHERIA, KANUNI ZA TUME
SALALI:Tunampongeza Rais Samia Kwa Kujumuisha Watu Wenye Ulemavu Dira 2050.
Rais Samia Azindua Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050, Asisitiza Utekelezaji Wa Vitendo Na Upimaji Wa Matokeo
IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.
AJIRA ZA MOJA KWA MOJA KATIKA SEKTA YA UTALII ZIMEONGEZEKA.
Uzalishaji wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 7.9 Hadi Tani 42.5
DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.
WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI.