Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama | The Dodoma Post
The Dodoma Post Nishati

Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezipongeza Kampuni za Total Ernergies na Super Star Fowarders – SSF kwa kuweza kufikia viwango vya juu vya usalama vya usafirishaji huku akiwataka wasafirishaji wengine kufuata nyayo zao kwa kuwa kampuni hizo ni mfano mzuri wa kuigwa

The Dododma Post
By The Dododma Post
25 Jun 2025
Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama

Dkt. Biteko amesema hayo Juni 25, 2025 jijini Dar es salaam wakati akishiriki katika maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya Kampuni ya Super Star Fowarders (SSF) na Total Energies.

 “ Leo tumekusanyika hapa kusherehekea hafla ya miaka 30 ya ushirikiano baina ya Kampuni zetu hizi mbili za Total Ernergies na Super Star Fowarders. Katika kipindi hicho chote, mmekuwa washirika wakubwa wa kimataifa katika usafirishaji wa bidhaa mbalimbali hususan kwa kutumia matenki maalum, hakika, binafsi nimefarijika sana  na hongereni sana” amesema Dkt. Biteko.

Amesema kupitia ushirikiano huo umewezesha  upatikanaji wa uhakika wa mafuta nchini na kutoa ajira kwa mamia ya vijana pamoja na  kuvutia nchi za jirani kutumia Bandari ya Dar Es Salaam kupitishia mizigo yao na kutoa fursa kwa Watanzania.

Ametoa wito kwa wasafirishaji wote wa mizigo kwa kutumia malori nchini wazingatie viwango  vya juu vya  usalama barabarani kwa kuhakikisha malori yao  yanawekwa vifaa vyote vya usalama kama vile GPS kufuata miongozoi liyopo.

Fauka ya hayo, Dkt. Biteko amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na wafanyabiashara wote na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kazi ikiwa ni pamoja na kuweka sera zenye kutabirika ambazo zitawalinda na kuvutia wawekezaji zaidi nchini.

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amewataka wasafirishaji kuzingatia usalama barabarani kwa kuwa suala hilo sio sera tu bali ni kwa maslahi mapana ya Taifa na  ajali za barabarani zinasababisha hasara kubwa ikiwemo uhai wa watu na uchumi wa nchi. Aidha, ametoa wito kwa wasafirishaji nchini kutumia barabara zilizopo kwa kuzingatia viwango.

Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Anne Sophie amesema siku hiyo ni muhimu kwa Tanzania na Ufaransa kwa kuadhimisha miaka 30  ya  ushirikiano kati ya kampuni hizo mbili ambao umekuwa na faida akitolea mfano mafunzo kwa madereva na matumizi ya  vifaa na mifumo ya kuzingatia usalama barabarani.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya Super Star Fowarders (SFF), Bw. Seif  A. Seif amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake na jitihada zinazosaidia kuimarisha na kukuza sekta ya usafirishaji nchini.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais Mwandamizi wa  Kampuni ya Total Energies Kanda ya Afrika – Huduma za Masoko, Bw. Jean Phillipe Torres ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na dhamira yake katika kuimarisha sekta ya nishati nchini.
 

REA Yashukuru Maono ya Rais Samia, Yajipanga Kusambaza Umeme na Nishati Safi Hadi Vitongojini

REA Yashukuru Maono ya Rais Samia, Yajipanga Kusambaza Umeme na Nishati Safi Hadi Vitongojini

EWURA YABORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWENYE MITANDAO YAO YA KIJAMII

EWURA YABORESHA UPATIKANAJI WA HUDUMA KWENYE MITANDAO YAO YA KIJAMII

NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.

NISHATI YA GESI ASILIA IMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KWA NCHI.

DKT. BITEKO AZINDUA MKAKATI WA TAIFA WA MAWASILIANO WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

DKT. BITEKO AZINDUA MKAKATI WA TAIFA WA MAWASILIANO WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

Morocco wampongeza Rais Samia kwa usimamizi bora Sekta ya Nishati

Morocco wampongeza Rais Samia kwa usimamizi bora Sekta ya Nishati