HAKUNA MWENYE MAMLAKA YA KUZUIA UCHAGUZI:VIJANA CCM. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

HAKUNA MWENYE MAMLAKA YA KUZUIA UCHAGUZI:VIJANA CCM.

Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM)wametoa onyo kwa wanaharakati na wanasiasa wasio na nia kwa taifa kuacha propaganda za upotoshaji kwani hakuna mwenye mamlaka ya kuzuia uchaguzi usifanyike hapa nchini.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
25 Jun 2025
HAKUNA MWENYE MAMLAKA YA KUZUIA UCHAGUZI:VIJANA CCM.

Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM)wametoa onyo  kwa wanaharakati na wanasiasa wasio na nia kwa taifa kuacha propaganda za upotoshaji kwani hakuna mwenye mamlaka ya kuzuia uchaguzi usifanyike hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya vijana CCM iliyopo Upanga jijini Dar es salaam mwanachama kijana Magula Marko Magula amesema kwamba hakuna mwananchi wala chama chochote chenye mamlaka kuzuia uchaguzi kwa kuwa uchaguzi ni swala la kikatiba na haki ya kila mwananchi

Aidha Magula ameongeza kuwa "Kila chama Cha siasa kina haki ya kushiriki au kutokushiriki uchaguzi hivyo kama kuna chama cha siasa hakijajipanga kuingia katika zoezi hili basi wasituharibie uchaguzi ".

Pia amewataka watanzania kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura na kuwataka vijana kuchukua fomu za kugombea nafasi mbali mbali za uongozi

Katika hatua nyingine kijana na mwanachama hai wa chama hicho ndugu Isaack Sumbaru amesema kuwa hakuna umma wowote utakaozuia uchaguzi kwani amani ndio tunu ya watanzania.

Aidha Isaack amesema kuwa " Niwahakikishie wananchi mabadiliko ya sheria ya uchaguzi yamefanyika kwa sababu kumekuwa na upotoshaji kwamba hakuna kilichofanyika na sote tukubaliane kwamba tume huru ya uchaguzi ipo kikatiba haijatungwa na mtu from nowhere na tume yetu ni miongoni mwa tume bora sana hapa Africa na Africa mashariki"

Pia Isaack ameongeza kuwa hapo awali tume ilikuwa hajiwezi kujiendesha yenyewe lakini hivi sasa inajiendesha kwa fedha za ndani,hivyo gharama zote zitagharamiwa na serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,vilevile utenda katika tume imeboreshwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali

Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja.

Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja.

TUME YASISITIZA UFANISI UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO

TUME YASISITIZA UFANISI UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA

ACT YAITAKA SERIKALI KUONDOA TOZO ZINAZOZUIA BIASHARA KUKUA .

ACT YAITAKA SERIKALI KUONDOA TOZO ZINAZOZUIA BIASHARA KUKUA .

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAVUNJWA KWA KISHINDO KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM.

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAVUNJWA KWA KISHINDO KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM.