TUME YASISITIZA UFANISI UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

TUME YASISITIZA UFANISI UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO

Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Magereza kwa Tanzania Bara na Vyuo vya Mafunzo kwa Tanzania Zanzibar wametakiwa kuzingatia mafunzo waliyopatiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ili waweze kutekeleza zoezi hilo kwa ufanisi.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
24 Jun 2025
TUME YASISITIZA UFANISI UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO

Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Magereza kwa Tanzania Bara na Vyuo vya Mafunzo kwa Tanzania Zanzibar wametakiwa kuzingatia mafunzo waliyopatiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ili waweze kutekeleza zoezi hilo kwa ufanisi.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa INEC, Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri mkoani Dodoma leo tarehe 24 Juni, 2025 wakati akifunga mafunzo kwa Waratibu, Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki wa magereza ya Tanzania Bara.

Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika sambamba na mafunzo ya watendaji wa vyuo vya mafunzo kwa upande wa Tanzania Zanzibar ikiwa ni maandalizi ya kuandikisha na kuboresha taarifa za mahabusu, wafungwa na wanafunzi waliohukumiwa kifungo chini ya miezi sita.

“Ikumbukwe kwamba, mafunzo na maelekezo mliyopewa ni zana muhimu za kuwawezesha kutekeleza kwa ufanisi majukumu yenu. Hivyo, mnatakiwa kuyafahamu vizuri na kuyafuata ili kutekeleza zoezi hili kwa ufanisi. Someni kwa makini vitabu vya maelekezo mlivyopatiwa ili kazi yenu ifanyike kwa usahihi,” amesema Mhe. Mapuri.

Amewasisitiza watendaji hao juu ya umuhimu wa kuwasiliana na waratibu kwa ajili ya ufafanuzi wa masuala yote yanayohusiana na utekelezaji wa majukumu yao.

Akifunga mafunzo kama hayo kwa watendaji wa vyuo vya mafunzo yaliyofanyika Kisiwani Unguja, Zanzibar, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari amewaasa watendaji hao kuhakikisha kuwa wanavitunza vizuri vifaa vya uboreshaji wa Daftari.

“Mnasisitizwa kuzingatia kwa umakini utunzaji wa vifaa vya uandikishaji kwa kuwa vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama kubwa sana. Kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa hivi kutapelekea athari kubwa ya vifaa hivyo muhimu kwa Taifa,” amesema Jaji Asina.

Amewakumbusha watendaji hao juu umuhimu wa kuzingatia muda sahihi wa kufungua na kufunga vituo vya kuandikisha wapiga kura na kuongeza kuwa watendaji hao wanapaswa kuwa na matumizi ya lugha nzuri kwa wale watakaowahudumia vituoni.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume, zoezi hilo la uboreshaji wa Daftari kwenye Magereza na Vyuo vya Mafunzo linafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 04 Julai, 2025 ambapo watakaohusika ni mahabusu na wafungwa walihukumiwa kifungo chini ya miezi sita.

Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja.

Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja.

HAKUNA MWENYE MAMLAKA YA KUZUIA UCHAGUZI:VIJANA CCM.

HAKUNA MWENYE MAMLAKA YA KUZUIA UCHAGUZI:VIJANA CCM.

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA

ACT YAITAKA SERIKALI KUONDOA TOZO ZINAZOZUIA BIASHARA KUKUA .

ACT YAITAKA SERIKALI KUONDOA TOZO ZINAZOZUIA BIASHARA KUKUA .

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAVUNJWA KWA KISHINDO KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM.

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAVUNJWA KWA KISHINDO KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM.