Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja.

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ametoa agizo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe kwamba vituo vyote vinavyotoa huduma za afya hapa nchini viweke wazi mikataba ya utoaji huduma bora kwa mteja ili kuepuka migogoro na migongano baina ya watoa huduma na wateja na pia akishangazwa na vitendo vya kuzuia maiti kwa madai ya madeni vilivyojitokeza kwa vipindi tofauti tofauti.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
25 Jun 2025
Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja.

Kauli hiyo ameitoa June 25 mwaka huu akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja katika ukumbi wa Wizara ya Afya Jijini Dodoma ambapo amesema mkataba huo ni ahadi baina ya Wizara ya Afya na Wananchi na unalenga kutoa huduma bora,sahihi na kwa wakati hivo kuleta mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma za afya hatua ambayo itaongeza uwajibikaji  kwa watendaji wa sekta hiyo.

"Na nyie mmeona wakati mwingine  kumekuwa na ugumu wa kutekeleza miongozo inayohusiana na huduma za hifadhi ya maiti,inabaki kuwa kelele maiti inashikiliwa eti inadaiwa,na ndio maana niliwaambia sasa maiti huyo kama alikuwa anajilipia mwenyewe matokeo yake ni nini? Tunataka afufuke ndo aende kujilipia?" Amesema Mhagama

Aidha ameagiza vituo vyote vinavyotoa huduma za afya vizingatie matumizi ya mifumo iliyowekwa kuhusiana na utoaji wa huduma za afya nchini  ili kupunguza malalamiko yasiyo ya msingi.

"Inakuwaje mgonjwa anaporuhusiwa ama kinapotokea kifo kituo cha kutolea huduma kinasema tunakudai, mgonjwa yeye anadai kwamba ameshalipa jambo gani limejificha na limejificha wapi? Tunataka watu wawe na mikataba na kila jambo liwe wazi ili tukiweza kutengeneza uwazi tutawabaini wale ambao hawana uwezo."Amesema Mhagama

Hata hivyo amesema kwamba huduma ambazo zimetajwa kwenye mkataba huo zinaendana na sera na miongozo mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za afya nchini,ushauri wa kitaalamu kuhusu uendeshaji wa shughuli za afya,maswala ya chanjo,vyeti vya usajili wa kitaaluma,leseni za kitaaluma,vibali mbalimbali,taarifa za sekta ya afya,mikataba ya kimataifa waliyoingia nayo,mikataba  ya ndani na huduma nyinginezo.

"Kupitia Mkataba huu wa huduma kwa mteja Wizara ya Afya niwahakikishie tumejipanga Vizuri kuyatekeleza hayo kwa ubora unaotakiwa." Amesema Mhagama

HAKUNA MWENYE MAMLAKA YA KUZUIA UCHAGUZI:VIJANA CCM.

HAKUNA MWENYE MAMLAKA YA KUZUIA UCHAGUZI:VIJANA CCM.

TUME YASISITIZA UFANISI UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO

TUME YASISITIZA UFANISI UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA

ACT YAITAKA SERIKALI KUONDOA TOZO ZINAZOZUIA BIASHARA KUKUA .

ACT YAITAKA SERIKALI KUONDOA TOZO ZINAZOZUIA BIASHARA KUKUA .

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAVUNJWA KWA KISHINDO KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM.

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAVUNJWA KWA KISHINDO KWA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM.