

Kwa mara nyingine, Ofisi ya Bunge imeandaa tamasha kabambe la michezo na burudani lijulikanalo kama Grand Bunge Bonanza linalotarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Viwanja vya S/Sekondari John Merlini, iliyopo Miyuji, Jijini Dodoma, Siku ya Jumamosi, Tarehe 21/06/2025 kuanzia Saa 12:00 asubuhi hadi Saa 6:00 mchana likiwa ni kubwa na mwisho katika Bunge hili la Kumi na Mbili.
Akizunguma na waandishi wa habari jijini hapa leo Juni 18 2025,Bungeni Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Festo Sanga amesema kuwa bonanza hilo mbali na kuwa na lengo la kuimarisha afya lakini pia ni kuleta mahusiano kati ya Bunge na Taasisi zingine za umma zitakazoshiriki katika bonanza hilo.
Aidha Bonanza hili limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Benki ya CRDB na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benki ya CRDB ikiwa ndiye Mdhamini Mkuu. Tamasha hili litabebwa na kauli Mbiu isemayo: “SHIRIKI UCHAGUZI MKUU, KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU”. Mgeni Rasmi katika Bonanza hili anatarajiwa Kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Bonanza hili linalohusisha Michezo mbalimbali ya ushidani kati ya Timu za Bunge na Taasisi nyingine za Serikali, pamoja na wadhamini wetu wakuu, lina lengo la kuwahamasisha Wabunge, Watumishi wa Ofisi ya Bunge na Wananchi kwa ujumla kushiriki katika michezo, ili kujenga Afya zao, kutoa burudani na pia kudumisha umoja na kujenga mshikamano miongoni mwetu"
Tamasha hilo kabambe litakuwa na michezo ya ushidani kati ya Timu za Bunge na Wadau Mbalimbali katika Michezo kama :Mpira wa Miguu: Bunge Vs CRDB, Mpira wa Pete :Bunge Vs PSSF, Kuvuta Kamba (Wanaume): Bunge Vs Maliasili & Utalii, Kuvuta Kamba (W/Wake) : Bunge Vs Uchukuzi, Mpira wa Kikapu (Wanaume) : Bunge Vs BOT, Mpira wa Kikapu (Wanawake) : Bunge Vs CRDB, Mpira wa Wavu (Wanaume) : Bunge Vs NSSF, Mpira wa Kikapu (Wanawake) : Bunge Vs UDOM
Aidha, Bonanza litajumuisha michezo mingine kama Mpira wa Meza; Pool Table; Kukimbia Riadha, Kutembea mwendo wa haraka; Kucheza Bao; Kucheza Draft; Kurusha Tufe; Kucheza Karata; mchezo wa Darts (Vishale) Kukimbia na Gunia; Kufukuza Kuku; Kujaza maji kwenye chupa kwa kutumia Kikombe; kushindana kunywa soda na kula chakula kwa haraka na Mchezo wa kushindana kuvaa Soksi.
"Kama ilivyoelezwa awali, Mdhamini Mkuu wa Bonanza hili ni Benki ya CRDB, ambao wamelipia gharama za vifaa vyote vya michezo, zikiwamo Medali, Tracksuits, T-shirts & Kofia kwa washiriki wote, Mipira ya Michezo mbalimbali, jezi za kila Mchezo utakaochezwa kama timu, hivyo tumekutana hapa pia kwa ajili ya kupokea Vifaa hivyo rasmi, na baadhi ya manahodha wa Timu tutakazoshindana nazo wapo hapa kuwawakilisha wenzao na pia kutoa hamasa ya Bonanza hili kubwa"
"Halikadhalika, wadhamini wetu wameandaa Kifungua kinywa kwa ajili ya Washiriki wote na tafrija jioni, ambayo pia itaambatana na burudani mbalimbali zikiwemo: Muziki wa Dansi; Ngoma za Asili na Utamaduni; Kughani ushairi; Muziki wa Taarabu na Ucheshi (Stand-up Comedy)"Ameongeza Sanga
"Kwa wakazi wa Jiji la Dodoma na Viunga vyake, karibuni Jumamosi kuanzia saa 1:00 asubuhi katika Viwanja vya Viwanja vya S/Sekondari John Merlini ili mjionee Mitanange ya nguvu kati ya Timu za Bunge na Wadau wetu mbalimbali kama nilivyoeleza awali"
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kutoka CRDB,Tully Mwambapa amesema kuwa benki hiyo imekuwa ikishirikiana kwa ukaribu na wabunge ambapo wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za kibenki pamoja na kudhamini mabonza ya kimichezo.
Aidha amesema kuwa Bonanza hilo litakuwa la kipekee kabisaa kwani wamejipanga kuhakikisha lina kuwa na mvuto wa aina yake yaani itakuwa kama festival Burudani za kutosha hivyo anawaalika wapenda michezo wote kujumuika katika Bonanza hilo.
"Kiukweli Bonanza hili litakuwa kama festival yaani tutacheza tutachoma nyama na kutakuwa na burudani mbalimbali hivyo njoo na familia yako yaaani huu ni mtoko maalumu wa kusherekea na familia"
KIHENZILE: UWAZI NA UWAJIBIKAJI NI NGUZO MUHIMU ZENYE TIJA KWA WANANCHI
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
ACT WAZALENDO KUUWASHA MOTO MANZESE WAJIDHATITI KUCHUKUA MAJIMBO YOTE DAR ES SALAAM
TANESCO YAJA NA KAMPENI MAALUM YA KUHAMASISHA ULIPAJI WA MADENI KWA WATEJA.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
VIJANA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA.
VIONGOZI WAANZA KUWAOGOPA WAJUMBE MOROGORO.
DODOMA YAELEKEA IRINGA KWA KISHINDO MASHINDANO YA UMISSETA.
Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto
TANZANIA KUWA MWENYEJI TUZO ZA 32 ZA KIMATAIFA ZA UTALII.