

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) George Katabazi, alisema kuwa mashindano ya Polisi Jamii Umoja Cup yamehusisha jumla ya timu 14 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa huo, kwa lengo la kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi.
Akizungumza wakati wa fainali ya Polisi Jamii Cup kati ya timu ya Mpunguzi na Chang’ombe, Katabazi alisema mashindano hayo si tu burudani bali pia ni chombo cha malezi ya uzalendo, nidhamu na ushiriki wa kijamii.
Alibainisha kuwa kupitia mashindano hayo, Jeshi la Polisi linakusudia kujenga uelewa na ushirikiano wa karibu na jamii ili kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vya kihalifu pamoja na kushiriki kikamilifu katika utoaji wa taarifa kuhusu uhalifu na wahalifu.
“Tunatumia michezo kama jukwaa la kuleta mshikamano, kuwahamasisha vijana kuepuka uhalifu na kuwa sehemu ya suluhisho kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kulinda amani ya maeneo yao,” alisema ACP Katabazi.
Kwa upande wake MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema michezo inaweza kuwa daraja muhimu la kuwahamasisha vijana kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia, hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
“Michezo siyo tu ushindani wa uwanjani. Ni darasa la maisha. Hapa vijana wanajifunza mshikamano, uvumilivu, na uzalendo—nguzo kuu za uchaguzi wa amani,” alisema RC Senyamule.
Aliongeza kuwa Serikali ya Mkoa wa Dodoma itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutumia michezo kama jukwaa la kutoa elimu ya uraia, kuhimiza usalama wa jamii na kuhamasisha vijana kujitokeza kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi.
“Rais Samia ameendelea kuwekeza kwa vijana kupitia michezo na programu mbalimbali. Tunapowaona vijana wakijitokeza kama hawa wa Polisi Jamii Cup, tunaona picha ya Taifa lenye matumaini,” alisema.
Aidha, aliwasihi vijana kutumia nafasi ya sasa sio tu kujiandikisha kama wapiga kura bali pia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, huku akisisitiza umuhimu wa kuepuka kauli na vitendo vinavyoweza kuvuruga amani.
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI