

Wazee wa Mkoa wa Dodoma waaswa kuhamasisha jamii kujitokeza Oktoba 29,2025 kupiga kura pamoja na kuhakikisha wanasimamia vijana na kuwasihi kulinda amani ya nchi yetu.
Wazee wa Mkoa wa Dodoma waaswa kuhamasisha jamii kujitokeza Oktoba 29,2025 kupiga kura pamoja na kuhakikisha wanasimamia vijana na kuwasihi kulinda amani ya nchi yetu.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule wakati akizungumza na Wazee hao leo Oktoba 09 juu ya umuhimu wao wa kuhamasisha jamii kujitokeza kupiga kura.
Aidha amesema kuwa ni jukumu la Kila mwananchi kuchagua viongozi wenye tija na maendeleo hivyo amewasihi wazee kuwa mstari wa mbele kwenye suala la uchaguzi kwani maendeleo yaliyofanywa na Serikali yanaonekana dhahiri.
Aidha amesema Dodoma ya miaka 10 iliyopita si sawa na Dodoma ya sasa kwani hata hadhi ya viwanja imeongezeka na kila mtu amekuwa akivutiwa na Dodoma hivyo anaipongeza Serikali kwa kufanya Dodoma kuwa ya kuvutia.
"Dodoma ya sasa si kama ya zamani Dodoma sasa inavutia na ni kimbilio la watanzania na wageni wa kimataifa kuwekeza Dodoma na hii ni kutokana na mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Serikali"Amesema Senyamule
Sanjari na hayo amesema kuwa Serikali imeamua kutoa Elimu juu ya magomjwa yasiyoambukizwa ili waweze kuhakikisha wazee wanakuwa imara kwenye Afya Kwa kufanya mazoezi na Kuzingatia mlo mzuri kulingana na umri wao.
"Kupitia nyie tutaweza kujua changamoto mlizonazo na kuweza kuhakikisha tunazitatua kwani wazee ni tunu ya taifa hili"Ameongeza Senyamule
Wazee hao nao walipata nafasi ya kuelezea changamoto zao Kwa Mkuu wa Mkoa wanazokumbana nazo kwenye huduma za Kijamii ikiwemo hospitali ambapo Mzee Bakari Chaurembo ameiomba Serikali kuwaangalia Kwa jicho la 3 Kwa kuhakikisha wanapatiwa Bima ya Afya ili waweze kupata huduma kwa urahisi na wakati kipindi wanapokwenda kwenye vituo vya Afya.
Akijibu hoja za wazee hao Mkuu wa Mkoa amesema atahakikisha anashughulikia changamoto zote ikiwemo huduma mbovu Kwa wazee kwenye vituo vya Afya,pamoja na kuboresha miundombinu kama barabara ili kuweza kukidhi matakwa ya Wazee hao.
"Kwenye ishu ya Wazee kutopanga foleni siku ya kupiga kura tutaliwasilisha Kwa TUME ya uchaguzi ili muweze kutengenezewa utaratibu mzuri"Amesisitiza Senyamule
Mfalme wa Mashairi Awasha Moto wa Uzalendo: “Kura Yako Ni Silaha”
MUFTI ATAKA WAISLAMU KUZINGATIA MAFUNDISHO YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29.
DOWOSA Yawaokoa Wanawake Dodoma Kutoka Mikononi mwa “Kausha Damu”
VIONGOZI WA DINI WAHIMIZA KUWAKATAA WASIOHESHIMU MISINGI NA TUNU ZA NCHI
Huduma za Uwakala CRDB Zachochea Ukuaji wa Mapato ya Serikali na Ujumuishi wa Kifedha
BADO TUNAMUHITAJI POLEPOLE KWA MKURUGENZI WA UPELELEZI- POLISI
BRIGEDIA JENERALI NDAGALA AFUNGUA KONGAMANO LA WADAU WA USIMAMIZI WA MAAFA JIJINI MBEYA
Mkomi Awasisitiza Wakuu wa Taasisi Kusimamia Mifumo ya Kielektroniki Serikalini.
JAMII YAHIMIZWA KUWAKATAA WANAOTAFUTA HAKI KWA KUVUNJA SHERIA
CRDB YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA HUKU WAKIJIVUNIA MAFANIKIO MAKUBWA KWA MIAKA 30