

SHABIKI maarufu wa Simba SC, Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula, ameonesha matumaini makubwa kwa timu yake licha ya kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya RS Berkane katika Uwanja wa Manispaa ya Berkane nchini Moroco.
Mabula, ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana,Mwanza amesema kuwa timu ya Simba ina uwezo wa kurekebisha makosa na kufanya vizuri katika mechi ya marudiano, akisisitiza kuwa mpira ni mchezo wa dakika 90 na kila mechi inaweza kubadilika.
"Tumepoteza mechi ya kwanza, lakini bado tunaamini kuwa tuna uwezo wa kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano. Kilichotokea Moroco hakitakuwa kikwazo hapa Tanzania. Simba ni timu kubwa, na tunajivunia kuwa na wachezaji bora ambao wanaweza kurejea kwa nguvu zaidi," amesema Mabula.
Mbunge Mabula ameongeza kuwa mabadiliko ya uwanja yanaweza kuwa na athari kwa utimamu wa wachezaji, lakini Simba kama timu kubwa, imejizatiti kwa mazoezi na maandalizi ambayo yatasaidia kufanya mabadiliko haya kuwa fursa badala ya changamoto.
Amesisitiza kuwa kwa kutumia uwanja wa nyumbani na ushawishi wa mashabiki, Simba ina nafasi nzuri ya kusonga mbele.
"Tuna imani kwamba kwa msaada wa mashabiki na uwanja wetu wa nyumbani, tutapata matokeo mazuri. Hii ni nafasi ya timu yetu kuonyesha uwezo wake na kutimiza malengo yake," amesema Mabula.
Hata hivyo shirikisho la soka Afrika(CAF) lilionyesha kuwa mchezo wa pili wa fainali ya kombe la shirikisho Afrika utachezwa kwenye uwanja wa New Amaan Complex,Zanzibar ambao ulitumika katika mchezo wa nusu fainali uliozikutanisha Simba na Stellenbosch ya Afrika kusini baada ya uwanja wa benjamini mkapa kuwa katika marekebisho.
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI