

KATIKA kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2025, Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI) imewahudumia zaidi ya wagonjwa 70 katika banda lao lililopo kwenye Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma, huku huduma nyingi zikitolewa kwa wagonjwa wa mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dkt. Tumaini Minja Daktari bingwa wa upasuaji mifupa MOI, amesema kuwa wagonjwa wengi waliowahudumia ni wenye matatizo ya maumivu sugu ya mgongo, magoti, nyonga na mishipa ya fahamu kwa ujumla, ambapo baadhi ni wagonjwa waliowahi kutibiwa MOI na wengine ni wapya waliopata huduma kwa mara ya kwanza wwngine wenyeji wa Dodoma na wanaotokea pembezoni .
“Wagonjwa wengi wanaotufikia ni wa umri kati ya miaka 45 hadi 60, na matatizo yao yanatokana zaidi na changamoto za umri, uzito mkubwa kupita kiasi, pamoja na mitindo ya maisha isiyojumuisha mazoezi ya mwili,” amesema Dkt. Minja.
Ameongeza kuwa magonjwa hayo yanatibika kulingana na hali ya mgonjwa, ambapo wengine huhitaji upasuaji na wengine hutibiwa kwa kutumia dawa au njia mbadala zisizo za upasuaji. Dkt. Minja amesema huduma wanazotoa kwenye maonesho hayo ni pamoja na uchunguzi wa awali, ushauri wa kitabibu na upangaji wa rufaa kwa matibabu zaidi MOI.
Aidha, MOI imejipanga kutoa huduma mahsusi kwa wanamichezo, kwani wengi wao hukumbwa na majeraha ya magoti,na viungo mbalimbali kutokana na shughuli zao.
Amesema kuwa changamoto kubwa kwa wanamichezo wengi ni kutofuata ushauri wa kitaalamu na kuchelewa kufika hospitali hadi hali inapoendelea kuwa mbaya.
“Tunawahamasisha wanamichezo wote kutembelea banda letu hapa Chinangali kwa ajili ya uchunguzi wa awali na kupata ushauri wa kiafya kabla ya majeraha kuwa makubwa. Matibabu si lazima yaanze baada ya maumivu, kinga ni bora zaidi,” amesisitiza.
Dkt. Minja amehitimisha kwa kuwakaribisha wakazi wa Dodoma na wageni wengine kutembelea banda la MOI ili kupata huduma na elimu kuhusu afya ya mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu, akibainisha kuwa taasisi hiyo itaendelea kushiriki kikamilifu katika kuimarisha huduma za afya nchini.
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
ACT WAZALENDO KUUWASHA MOTO MANZESE WAJIDHATITI KUCHUKUA MAJIMBO YOTE DAR ES SALAAM
TANESCO YAJA NA KAMPENI MAALUM YA KUHAMASISHA ULIPAJI WA MADENI KWA WATEJA.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 107 ZAKAMILISHA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI SIMIYU
VIJANA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA.
VIONGOZI WAANZA KUWAOGOPA WAJUMBE MOROGORO.
DODOMA YAELEKEA IRINGA KWA KISHINDO MASHINDANO YA UMISSETA.
Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto
TANZANIA KUWA MWENYEJI TUZO ZA 32 ZA KIMATAIFA ZA UTALII.