

Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Wizara ya Nishati imetumia takribani shilingi bilioni 107.36 kupeleka umeme kwenye Vijiji vyote 474 vya Mkoa wa Simiyu.
*Kapinga asema sasa Serikali inapeleka umeme kwenye Vitongoji 638*
*Ataja miradi ya kuimarisha umeme Simiyu*
*Simiyu yapata mitungi ya gesi 16,275 kwa bei ya ruzuku*
Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Wizara ya Nishati imetumia takribani shilingi bilioni 107.36 kupeleka umeme kwenye Vijiji vyote 474 vya Mkoa wa Simiyu.
Kapinga ameyasema hayo leo Juni 18, 2025 wakati akitoa tathmini ya hali ya upatikanaji wa umeme Mkoa wa Simiyu na maendeleo ya usambazaji wa nishati safi ya kupikia wakati wa kuhitimisha ziara ya kikazi ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Simiyu.
"Mheshimiwa Rais baada ya kumaliza upelekaji wa umeme kwenye Vijiji, hivi sasa tunapeleka umeme kwenye Vitongoji na hivi sasa tunatekeleza miradi ya umeme kwenye Vitongoji 638 kati ya Vitongoji 1,408 vya Mkoa wa Simiyu”. Amesema Mhe. Kapinga
Ameongeza kuwa Serikali itajenga kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Simiyu kupitia mradi wa gridi imara na kuongeza kuwa hivi sasa Mkoa wa Simiyu unapata huduma ya umeme kutoka Mikoa mitatu ya Shinyanga, Mwanza na Mara.
Amesema kituo hicho kitazidi kuimarisha hali ya umeme Simiyu na hivyo kuwa muhimu kwa maendeleo ya watu wa Simiyu.
Amesema mradi wa gridi imara mkoani Simiyu una sehemu mbili ambazo ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Ibadakuli Shinyanga hadi Bariadi utakaojengwa kwa takribani shilingi bilioni 48 na ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Bariadi kitakachojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 49.
Ameongeza kuwa, kukamilika kwa mradi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme Mkoa wa Simiyu utawezesha Mkoa kuwa na uwezo wa megawati 150.
Kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, Kapinga amesema Mkoa wa Simiyu umepata mitungi ya gesi ya ruzuku takribani 16,275 ambayo yote tayari imeshachukuliwa na wananchi kwa bei ya ruzuku.
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI