VIJANA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

VIJANA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA.

Vijana Wanaotumia vibaya mitandao ya Kijamii waonywa na kuaswa kuacha mara moja na kutumia mitandao hiyo kujifunza na kujikwamua kiuchumi na kuacha matusi na uchochezi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
11 Jun 2025
VIJANA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma nakusema amewaonya watu wote wanaopotosha umma kwani serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria hususani vijana wanaotumia mitandao Kwa njia zisizofaa.

Aidha Msigwa, amewaonya vijana wa vyuo vikuu kuacha kutumika kuichafua serikali kwa kuandika  mambo ambayo yanaigombanisha serikali na wananchi wake.

“Nitumie fursa hii kuwaonya vijana wetu wa vyuo vikuu kuacha kutumia mitandao ya kijamii kuichafua serikali bali watumie kwa manufaa yao wenyewe ikiwemo kujifunza, kujielimisha na kama vijana wafanya biashra basi watumiwe mitandao hiyo kutangaza biasahra zao badala ya kufanya vitu ambavyo vinaweza kuwaingiza matatizoni kwani sheria ipo na vyombo vya dola vipo na  wengi ambao tumekuwa tukiwakamata wanasema walikuwa hawajui lakini kutokujua siyo sababu ya kuvunja sheria” Amesema

Katika hatua nyingine Msigwa amesema Tanzania imeandika historia kwa kupokea gawio kutoka kwa mashirika ya umma ya sh.trilioni 1.28

Amesema kuongezeka kwa gawio hilo kunatokana na utashi wa serikali ya Awamu ya Sita ya kuongeza uwekezaji katika mashirika ya umma hadi kufikia sh.trilioni  86.

Vilevile amesema kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika mashirika ya umma gawio la serikali litaendelea kuongezeka.

Msigwa amesema kuongezeka kwa fedha hizo pia kunatokana na kutumika kwa 4R zilizoasisiwa na Rais Dk.Samia.

“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia imeandika historia kwa kupokea gawio la zaidi ya sh.trilioni 1.28 kutoka kwa mashirika ya umma ambayo serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa sh.trilioni 86.
Ameongeza kuwa :”Kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika tunaamini gawio kwa serikali litaendelea kuongezeka miaka kwa miaka,”.

Sanjari na hayo amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku saba katika mikoa ya Simiyu na Mwanza ambapo atazungumza na wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Daraja la Kigongo Busisi.

Amesema Rais Dkt.Samia atawasili mkoani Simiyu Juni 15 mwaka huu ambapo atazungumza  na wananchi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Juni 19 mwaka huu atawasili mkoani Mwanza atazindua daraja la Kigongo-Busisi ambalo tayari limekamilika kwa asilimia 100. Kukamilika kwa daraja hilo ni historia ambayo imewekwa na serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia,” Amesema

Vilevile amesema Rais Dkt.Samia amepata mualiko maalum na atafanya ziara ya kikazi katika nchi ya Msumbiji na Visiwa vya Comoro.

Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto

Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto

VIONGOZI WAANZA KUWAOGOPA WAJUMBE MOROGORO.

VIONGOZI WAANZA KUWAOGOPA WAJUMBE MOROGORO.

SPIKA WA BUNGE DK TULIA AWATAKA VIJANA WA VYUO KUJITOKEZA KUPIGA KURA OCTOBA NA KUMCHAGUA RAIS DK SAMIA.

SPIKA WA BUNGE DK TULIA AWATAKA VIJANA WA VYUO KUJITOKEZA KUPIGA KURA OCTOBA NA KUMCHAGUA RAIS DK SAMIA.

Rais Samia Asisitiza Mchujo wa Wagombea Kufanyika Kwa Haki.

Rais Samia Asisitiza Mchujo wa Wagombea Kufanyika Kwa Haki.

WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE SABA

WIZARA YA ARDHI YAJA NA VIPAUMBELE SABA