BRELA yatoa Gawio la Shilingi Bilioni 20.4 kwa Serikali | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

BRELA yatoa Gawio la Shilingi Bilioni 20.4 kwa Serikali

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa gawio la Shilingi Bilioni 20.4 kwa Serikali kwa mwaka 2025, likiwa ni ongezeko kutoka Shilingi Bilioni 18.9 zilizotolewa mwaka 2024.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
10 Jun 2025
BRELA yatoa Gawio la Shilingi Bilioni 20.4 kwa Serikali

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa gawio la Shilingi Bilioni 20.4 kwa Serikali kwa mwaka 2025, likiwa ni ongezeko kutoka Shilingi Bilioni 18.9 zilizotolewa mwaka 2024.

Gawio hilo limetolewa leo JUNE 10, Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma.

Vilevile, BRELA imepokea tuzo kama Taasisi iliyofanya vizuri katika kuchangia gawio kila mwaka, kwa wastani wa Shilingi Bilioni 16.8 kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi husika, wakiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya BRELA, Prof. Neema Mori, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa.

HISTORIA YAANDIKWA RAIS DK.SAMIA APOKEA SH.TRILIONI 1 KAMA GAWIO NA MICHANGO MINGINE.

HISTORIA YAANDIKWA RAIS DK.SAMIA APOKEA SH.TRILIONI 1 KAMA GAWIO NA MICHANGO MINGINE.

TUME YA UCHAGUZI YAPONGEZWA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2025

TUME YA UCHAGUZI YAPONGEZWA MAANDALIZI UCHAGUZI MKUU 2025

Rais Samia kupokea gawio la kihistoria, wachumi watarajia makubwa

Rais Samia kupokea gawio la kihistoria, wachumi watarajia makubwa

VITONGOJI 284 ARUMERU MASHARIKI VYAFIKIWA NA UMEME

VITONGOJI 284 ARUMERU MASHARIKI VYAFIKIWA NA UMEME

RAIS SAMIA Ni Mkombozi wa Maendeleo katika Nchi yetu:Mmuya

RAIS SAMIA Ni Mkombozi wa Maendeleo katika Nchi yetu:Mmuya