

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar Mmuya amesema Rais Samia ni Mkombozi wa Maendeleo katika Nchi yetu kwani katika kipindi chake wananchi wamepata mahitaji muhimu kama barabara,maji, umeme,afya na Elimu.
Mmuya amesema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa kata ya Zanka wilaya ya bahi ikiwa ni maadhimisho ya Samia Day kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kipindi Cha miaka minne ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Ameongeza kuwa katika kata ya Zanka pekee Rais ametoa Shilingi bilioni 8 kati ya Bilioni 52 zilizotolewa kwenye wilaya ya Bahi na vitongoji vyake kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wilaya hiyo.
"Tumekutana kwa ajili ya kumshukuru Rais Samia kwa ajili ya mambo makubwa ambayo ameyafanya katika nchi hii,tumesema mafanikio haya yasisimuliwe tu mkoani bali tuingie ngazi za kata na wananchi waweze kutoa ushuhuda wa yale aliyoyafanya Mhe.Rais"Amesema Mmuya
"Tumeshuhudia hospitali mpya ya wilaya ambapo miradi mingi ya umeme imefika katika vijiji vitatu vya Zanka na niwahakikishie kupitia programu ya REA umeme utafika vijiji vichache ambavyo bado havina umeme"
Naye Lister Ulalo mwananchi wa kata hiyo amemshukuru Rais kwa kumtua mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha Zanka matenki yametengenezwa na yanakarabatiwa vizuri bila kusahau mradi wa kusaidia kaya maskini(TASAF) kila kijiji wamepata fedha na wamerahisisha mfumo hadi kwenye sim.
"Tunamshukuru Rais kwa kutuletea hospitali za Kisasa hadi vijijini wamama wanajifungua Kwa kutumia vifaa vya kisasa hivyo tunamshukuru Rais kwa kuifanya Zanka kuwa ya Kisasa"Amesema Bi.Fatuma Vicent kutoka Kijiji cha Mkondai
Gilbert Kizenga Mwakilishi wa Wazee kata ya Zanka amesema walikuwa hawaoni kutoka mayamaya kwenda Mkondai ila sasa hivi umeme Kila mahali,hata majambazi wanaogopa kuingia vijijini kwa sababu ya Nuru.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Joachim Thobias amesema wamekusanyika kuelezea mazuri yanayofanywa na Rais ambapo bahi na vitongoji vyake vimeguswa na Shilingi bilioni 52.
Ambapo Bilioni 7 zimetolewa katika kata ya Babayu iliyopelekwa kwenye miradi ya maendeleo ya kata hiyo na nimatumaini yake wananchi wote wa Wilaya ya Bahi wameona juhudi za Mhe.Rais
"Nitoe Rai Kwa wananchi kutumia vizuri fursa zinazotolewa na kiongozi wetu pamoja na kulinda amani bila kusahau kushiriki kikamilifu katika uchaguzi Mkuu"
DODOMA YAELEKEA IRINGA KWA KISHINDO MASHINDANO YA UMISSETA.
Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto
VIJANA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA.
VIONGOZI WAANZA KUWAOGOPA WAJUMBE MOROGORO.
TANZANIA KUWA MWENYEJI TUZO ZA 32 ZA KIMATAIFA ZA UTALII.
HANANJA AWAONYA VIONGOZI WA DINI WANAOTUMIA MAJUKWAA YA DINI KUPOTOSHA UMMA.
HISTORIA YAANDIKWA RAIS DK.SAMIA APOKEA SH.TRILIONI 1 KAMA GAWIO NA MICHANGO MINGINE.
Waziri Mhagama amewataka kina Mama kuwa makini na Bidhaa Wanazotumia wakati wa Hedhi.
VIJANA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA.
Rais Samia kupokea gawio la kihistoria, wachumi watarajia makubwa