Waziri Mhagama amewataka kina Mama kuwa makini na Bidhaa Wanazotumia wakati wa Hedhi. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

Waziri Mhagama amewataka kina Mama kuwa makini na Bidhaa Wanazotumia wakati wa Hedhi.

Waziri wa Afya, Mheshimiwa Jenista Mhagama amesema Katika kuimarisha afya ya wanawake, amewataka akinamama hususani walioko katika hedhi au waliokwisha jifungua kuwa makini na bidhaa wanazotumia, akisisitiza umuhimu wa kutumia bidhaa zilizoidhinishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kuepuka maambukizi hatarishi.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
09 Jun 2025
Waziri Mhagama amewataka kina Mama kuwa makini na Bidhaa Wanazotumia wakati wa Hedhi.

Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa vifaa kwa wakina mama na watoto vilivyotolewa na kampuni ya Doweicar technology company  LTD Waziri Mhagama ameeleza kuwa matumizi ya bidhaa zisizokidhi viwango yanaweza kusababisha maambukizi ya njia ya mkojo (UTI), ambayo huweza kusababisha madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kuathiri figo.

“Napenda kuwasihi akinamama kutumia bidhaa bora na salama kama vile pedi za SOFTCARE ambazo zimethibitishwa na Shirika la viwango Tanzania (TBS)
Bidhaa hizi siyo tu zina viwango bali pia zinasaidia kupunguza hatari ya kupata UTI, ambayo ikiambatana na kuchelewa kutibiwa, inaweza kusababisha matatizo ya figo,” amesema Waziri.

Aidha, ametoa rai kwa wazazi, walezi, na jamii kwa ujumla kuendelea kuelimishana juu ya umuhimu wa usafi wa mwili, hasa kwa wanawake na wasichana, ili kuhakikisha taifa lina kizazi chenye afya bora.

Aidha amesema kuwa ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza (Non-Communicable Diseases - NCDs) kama vile kisukari, shinikizo la damu, na matatizo ya figo, limeendelea kuwa changamoto kubwa kwa serikali kutokana na gharama kubwa za matibabu zinazohitajika kuyakabili.

"magonjwa hayo si tu yanatishia ustawi wa jamii bali pia yanachangia kwa kiasi kikubwa matumizi makubwa ya rasilimali za serikali kwenye sekta ya afya"

"Ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza linazidi kuongeza mzigo kwa serikali. Hali hii inatufanya tuimarishe zaidi juhudi za kinga na kuhimiza wananchi kuchukua hatua za mapema za kujilinda na magonjwa haya," amesema Mhagama.

Kwa upande wake, Balozi wa Softcare, Zari The Boss Lady,  amewasihi kina mama kuendelea kutumia pedi za kampuni hiyo kwani zimetengenezwa kwa pamba halisi na ni rafiki kwa mama awapo kwenye siku zake. Kwa watoto wadogo pia ni rafiki na hazichubui, hivyo kumfanya mtoto kuwa huru wakati wote.

"Pedi hizi ni nzuri na ni rafiki wa mazingira hivyo, nawasihi kina mama wenzangu kuifanya kuwa chaguo lao la kwanza, kwani hazichubui na ni salama kwa afya ya kila mwanamke anapokuwa kwenye siku zake, na salama zaidi kwa watoto," amesema Zari.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema anawashukuru Softcare kwa kuweza kuwafikia kina mama wa Mkoa wa Dodoma, na amefurahishwa kujua kuwa kampuni hiyo imethibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na kwamba bidhaa zake ni nzuri kwa kina mama na watoto bila kuleta madhara ya kiafya.

HANANJA AWAONYA VIONGOZI WA DINI WANAOTUMIA MAJUKWAA YA DINI KUPOTOSHA UMMA.

HANANJA AWAONYA VIONGOZI WA DINI WANAOTUMIA MAJUKWAA YA DINI KUPOTOSHA UMMA.

DMI YATOA ELIMU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MAJINI JIJINI DODOMA

DMI YATOA ELIMU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MAJINI JIJINI DODOMA

Makamu wa Rais Dkt.Mpango Ametoa Wito Kwa Wadau wa Mazingira Kuendeleza Utunzaji wa Mazingira.

Makamu wa Rais Dkt.Mpango Ametoa Wito Kwa Wadau wa Mazingira Kuendeleza Utunzaji wa Mazingira.

Mila Zinavyogeuka Mtego wa Maisha kwa Watoto wa Chemba

Mila Zinavyogeuka Mtego wa Maisha kwa Watoto wa Chemba

SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA

SERIKALI NA WADAU WAENDELEZA MAPAMBANO YA KIJINSIA