

Ikiwa ni mara ya pili tangu Sheikh Ponda Issa Ponda alipotangaza kujiunga na Chama cha ACT WAZALENDO,Umati wa wananchi wahudhuria hadhara ya kisiasa iliyoandaliwa na Chama hicho June,18 2025 iliyofanyika katika viwanja vya Bakharesa Manzese jijini Dar es salaam
Ikiwa ni mara ya pili tangu Sheikh Ponda Issa Ponda alipotangaza kujiunga na Chama cha ACT WAZALENDO,Umati wa wananchi wahudhuria hadhara ya kisiasa iliyoandaliwa na Chama hicho June,18 2025 iliyofanyika katika viwanja vya Bakharesa Manzese jijini Dar es salaam
Akizungumza mbele ya wananchi na waandishi wa habari Sheikh Ponda ameeleza namna watanzania wanavyoweza kuleta mabadiliko makubwa endapo watashiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura,
"Tunachokifanya sisi ni kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kusimama na kuwa tayari kupiga kura na kulinda kura kwa sababu wabunge wote wa vyama vya upinzani wanaoingia bungeni ulitumika misuli ya wananchi katika kuhakikisha kwamba yule anayepata ridhaa ya wananchi ndiye anayetangazwa"
Pia amebainisha baadhi ya changamoto katika sekta ya afya hususan gharama kubwa wanazotoa waathirika wa magonjwa ya figo katika zoezi la kusafisha damu
"Ndugu zangu hakuna ubinadamu katika eneo la sekta ya afya,mtu figo zake zikifeli anatakiwa kutoa 180000 mara tatu kwa wiki na asipotoa anaambiwa arudi nyumbani matokeo yake mgonjwa anakufa kizembe"
Katika hatua nyingine Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Isihaka Mchinjite ameuhamasisha umma kuungana ili kuleta matokeo chanya katika nchi
Aidha Naibu Katibu Mkuu Bw Ado Shaibu alihitimisha kwa kubainisha lengo la kuanza kufanya hadhara zao katika mkoa wa Dar es Salam ikiwa ni kwa kuwa Jiji la Dar es salaam ni kitovu cha mikosa yote hapa nchini hivyo wanaamini zitaleta matokeo makubwa.
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI