

Shirika la umeme nchini TANESCO limeanza rasmi kampeni maalum ya kuhamasisha ulipaji wa madeni kwa wateja wa malipo ya baada lakini pia ukaguzi wa mita za luku kwa wateja wa malipo ya kabla.
Shirika la umeme nchini TANESCO limeanza rasmi kampeni maalum ya kuhamasisha ulipaji wa madeni kwa wateja wa malipo ya baada lakini pia ukaguzi wa mita za luku kwa wateja wa malipo ya kabla.
Akizungumza na waandishi wa habari leo juni 19,2025 Jijini Dar es salaam kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na huduma kwa wateja Irene Gowele amesema kampeni hiyo imeanza rasmi leo Juni 19,2025 ambayo imepewa jina la 'lipa deni,linda miundombinu tukuhudumie' ambapo kauli mbiu ya kampeni hiyo ikiwa 'huduma endelevu huanza na wewe'.
Amesema malengo ya kampeni hiyo ni pamoja na kuwahamsisha wateja wa malipo ya baada kulipa madeni yao hiyari kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.
"Tunawahamasisha wateja wa malipo ya baada kulipa madeni yao kwa hiyari kabla ya kuchukua hatua za kisheria lakini pia tunatoa motisha kwa ulipaji kwa wakati ikiwemo msamaha wa riba kwa wateja watakaolipa madeni yao kikamilifu",Amesema.
Aidha ameongeza kuwa zoezi hilo litaenda sambamba na kuhamasisha ulinzi wa miundombinu ya umeme ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha na kuimarisha uendelevu wa upatikanaji wa huduma bora ya umeme kwa wananchi.
Amesema zoezi hilo litahusisha pia ukaguzi wa mita za luku lengo likiwa kuhakisha luku zinafanya kazi vizuri na hazijachezewa na wateja wasio waaminifu.
"Tunatoa elimu kwa wananchi jinsi ya kulinda miundombinu ya shirika kwani hii miundombinu ndio inayowezesha upatikanaji endelevuwa huduma ya umeme kwa ufanisi kwa kuzingatia kwamba ulinzi wa miundombinu ya umma ni wajibu wa kila mwananchi ",amesema.
Hivyo TANESCO inatoa rai kwa wateja na wananchi wote wanaodaiwa kutoa ushirikiano kwa kulipa madeni yao kwa wakati lakini pia kutoa taarifa kuhusu vitendo vya wizi wa umeme au uharibifu na wizi wa miundombinu ya umeme kwa kushirikiana na vyombo vya dola ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kwa ukosefu wa huduma ya umeme pamoja na kuzuia hasara kwa shirika.
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI