

Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2025, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile (Mb), ametembelea banda la Wizara ya Uchukuzi katika Viwanja vya Chinangali Dodoma, ambapo amepongeza jitihada za watumishi wa sekta hiyo kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza na watendaji wa wizara hiyo, leo June 19,2025 Kihenzile amesema Wiki ya Utumishi wa Umma ni fursa muhimu ya kujifunza, kusikiliza wananchi, na kuboresha mifumo ya utoaji huduma, hasa katika sekta ya uchukuzi ambayo ndiyo mhimili wa maendeleo ya kiuchumi.
“Sekta ya uchukuzi inagusa maisha ya kila Mtanzania iwe ni kwenye reli, barabara, anga au usafiri wa majini tunahitaji kuendelea kujenga mfumo unaomuweka mwananchi mbele kwa kuhakikisha huduma ni za haraka, salama, na zenye tija,” amesema.
Ameongeza kuwa maonesho hayo yanaongeza uwazi na uelewa kwa wananchi kuhusu huduma zinazotolewa na Wizara ya Uchukuzi, sambamba na kuwaweka karibu zaidi na Serikali yao.
“Katika wiki hii, tunapaswa kujiuliza kama tunamtumikia mwananchi kwa uadilifu na ufanisi,Watumishi wa umma tuna jukumu la kuakisi maadili ya uwajibikaji, uvumilivu na ubunifu kwa manufaa ya Taifa letu,” amesisitiza Kihenzile.
Ziara ya Naibu Waziri imeleta hamasa kwa wadau waliotembelea banda hilo, huku watendaji wa wizara wakiahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa kuzingatia dira ya maendeleo ya uchumi wa viwanda na usafirishaji endelevu.
KIHENZILE: UWAZI NA UWAJIBIKAJI NI NGUZO MUHIMU ZENYE TIJA KWA WANANCHI
ACT WAZALENDO KUUWASHA MOTO MANZESE WAJIDHATITI KUCHUKUA MAJIMBO YOTE DAR ES SALAAM
TANESCO YAJA NA KAMPENI MAALUM YA KUHAMASISHA ULIPAJI WA MADENI KWA WATEJA.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 107 ZAKAMILISHA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI SIMIYU
VIJANA WANAOTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII WAONYWA.
VIONGOZI WAANZA KUWAOGOPA WAJUMBE MOROGORO.
DODOMA YAELEKEA IRINGA KWA KISHINDO MASHINDANO YA UMISSETA.
Serikali Yatangaza Kuanza Msako Kuwabaini Wanaotumikisha Watoto
TANZANIA KUWA MWENYEJI TUZO ZA 32 ZA KIMATAIFA ZA UTALII.