Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake

Dodoma. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya imezindua rasmi kampeni ya INSPIRE TO LEAD yenye lengo la kubadilisha fikra na mitazamo ya jamii kuhusu usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika nafasi za uongozi.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
25 Jun 2025
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake

Uzinduzi huo umefanyika leo, Juni 25, 2025, jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo maafisa habari kutoka wizara mbalimbali, wawakilishi wa mashirika ya kiraia, wanafunzi na wanaharakati wa masuala ya kijinsia.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima amesema kampeni hiyo inalenga pia kuongeza hali ya kujiamini kwa wanawake na wasichana pamoja na kuwawezesha kushiriki katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM).

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima akizungumza katika uzindua rasmi wa kampeni ya INSPIRE TO LEAD yenye lengo la kubadilisha fikra na mitazamo ya jamii kuhusu usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika nafasi za uongozi.

“Hatuna budi kushirikiana kwa pamoja kwani kampeni hii si ya Wizara moja au Serikali pekee, ndiyo maana tumewaalika wadau mbalimbali ili kwa pamoja tujenge jamii yenye usawa wa kijinsia,” amesema Dk. Gwajima.

Ameeleza kuwa kupitia kampeni hiyo, Serikali inatarajia kuona matokeo chanya katika kipindi cha miaka michache ijayo ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanawake katika nafasi za uongozi, hususan katika sekta ambazo awali zimekuwa zikitawaliwa na wanaume kama vile uhandisi, madini na urubani.

Ofisa Habari TASAFU Bi. Samira Kiango akiwa katika uzindua rasmi wa kampeni ya INSPIRE TO LEAD yenye lengo la kubadilisha fikra na mitazamo ya jamii kuhusu usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika nafasi za uongozi.

“Uelewa wa jamii kuhusu usawa wa kijinsia utaongezeka, vitendo vya ukatili vitaendelea kupungua na idadi ya wasichana wanaojiunga na masomo ya STEM itaongezeka,” amesema.

Waziri Gwajima ametoa wito kwa washiriki wote wa kampeni hiyo kuhakikisha ujumbe unawafikia walengwa kwa usahihi ili kuijenga jamii yenye uelewa, wanawake jasiri na wasichana wenye uthubutu wa kuchukua mwelekeo wa sayansi na teknolojia kwa maendeleo ya taifa.

Kampeni ya INSPIRE TO LEAD ni sehemu ya jitihada za Serikali na wadau wa maendeleo katika kufikia usawa wa kijinsia na kujenga jamii jumuishi yenye fursa sawa kwa wote.

Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma

Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma

Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja

Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja

CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA VINARA WA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME NA KUDUMISHA AMANI KWENYE MITAA YAO.

CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA VINARA WA ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME NA KUDUMISHA AMANI KWENYE MITAA YAO.

Waziri Mkuu Azindua Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini GovESB.

Waziri Mkuu Azindua Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini GovESB.

LUKUVI AWASILISHA BUNGENI TAARIFA YA HALI YA DAWA ZA KULEVYA

LUKUVI AWASILISHA BUNGENI TAARIFA YA HALI YA DAWA ZA KULEVYA