

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ametoa agizo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe kwamba vituo vyote vinavyotoa huduma za afya hapa nchini viweke wazi mikataba ya utoaji huduma bora kwa mteja ili kuepuka migogoro na migongano baina ya watoa huduma na wateja na pia akishangazwa na vitendo vya kuzuia maiti kwa madai ya madeni vilivyojitokeza kwa vipindi tofauti tofauti.
Kauli hiyo ameitoa June 25 mwaka huu akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja katika ukumbi wa Wizara ya Afya Jijini Dodoma ambapo amesema mkataba huo ni ahadi baina ya Wizara ya Afya na Wananchi na unalenga kutoa huduma bora,sahihi na kwa wakati hivo kuleta mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma za afya hatua ambayo itaongeza uwajibikaji kwa watendaji wa sekta hiyo.
"Na nyie mmeona wakati mwingine kumekuwa na ugumu wa kutekeleza miongozo inayohusiana na huduma za hifadhi ya maiti,inabaki kuwa kelele maiti inashikiliwa eti inadaiwa,na ndio maana niliwaambia sasa maiti huyo kama alikuwa anajilipia mwenyewe matokeo yake ni nini? Tunataka afufuke ndo aende kujilipia?" Amesema Mhagama
Aidha ameagiza vituo vyote vinavyotoa huduma za afya vizingatie matumizi ya mifumo iliyowekwa kuhusiana na utoaji wa huduma za afya nchini ili kupunguza malalamiko yasiyo ya msingi.
"Inakuwaje mgonjwa anaporuhusiwa ama kinapotokea kifo kituo cha kutolea huduma kinasema tunakudai, mgonjwa yeye anadai kwamba ameshalipa jambo gani limejificha na limejificha wapi? Tunataka watu wawe na mikataba na kila jambo liwe wazi ili tukiweza kutengeneza uwazi tutawabaini wale ambao hawana uwezo."Amesema Mhagama
Hata hivyo amesema kwamba huduma ambazo zimetajwa kwenye mkataba huo zinaendana na sera na miongozo mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za afya nchini,ushauri wa kitaalamu kuhusu uendeshaji wa shughuli za afya,maswala ya chanjo,vyeti vya usajili wa kitaaluma,leseni za kitaaluma,vibali mbalimbali,taarifa za sekta ya afya,mikataba ya kimataifa waliyoingia nayo,mikataba ya ndani na huduma nyinginezo.
"Kupitia Mkataba huu wa huduma kwa mteja Wizara ya Afya niwahakikishie tumejipanga Vizuri kuyatekeleza hayo kwa ubora unaotakiwa." Amesema Mhagama
Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja.
Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
HAKUNA MWENYE MAMLAKA YA KUZUIA UCHAGUZI:VIJANA CCM.
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.
PPAA yatoa elimu matumizi ya Moduli Wiki ya Utumishi wa Umma