

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndugu Albert Chalamila ametoa rai kwa wenyekiti wa serikali za mitaa na watendaji wake kutambua umuhimu wa kulilinda taifa lao kwani wao ndio wenye dhamana ya kuhakikisha wanatetea ulinzi na amani
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndugu Albert Chalamila ametoa rai kwa wenyekiti wa serikali za mitaa na watendaji wake kutambua umuhimu wa kulilinda taifa lao kwani wao ndio wenye dhamana ya kuhakikisha wanatetea ulinzi na amani.
Rai hiyo aliitoa Leo June 24 2025 katika kikao cha shirika la umeme TANESCO na wenyekiti wa serikali za mitaa halmashauri ya Kinondoni na Ubungo pamoja na watendaji mbali mbali katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es salaam
"Mara nyingi watendaji wa serikali wanazungumzia madili na faida wanazozipata kwenye uongozi bila kujali usalama wa mitaa yao lakini kama ninyi hamtakua wasimamizi wazuri katika mitaa yenu mshahara wa uzembe unaweza kuwadondokea ninyi wenyewe viongozi wa serikali za mitaa" alisema Chalamila
Aidha kiongozi huyo ameeleza kuwa shirika la umeme TANESCO limefanya kazi kubwa katika kuzuia wizi wa mafuta pamoja na ushushaji wa transifoma hivyo amewataka watendaji hao kusimamia ulinzi wa miundombinu ya umeme katika mitaa yao .
Katika hatua nyingine mkurugenzi wa TANESCO Bw.Lazaro Twagi amezungumza kuwa swala la utekelezaji wa miradi ya umeme uko kwenye mkono wa serikali za mitaa kwa sababu wananchi ndio wateja wakuu wa umeme hivyo amedhamiria kutengeneza mfumo mzuri wa mawasiliano ili kuboresha huduma zao.
Mkurugenzi ametoa wito kwa viongozi hao kuwa daraja kati yao na wananchi hususan pale wananchi wanapohitaji kupata taarifa juu ya miradi ya shirika hilo
Katika kutengeneza urafiki wa kistratejia shirika la umeme limeweka dhamira ya dhati ya kuwafikia wenyeviti wote nchini ili kusikia sauti za wananchi juu ya huduma zao
Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja.
Wenye malori watakiwa kuweka vifaa vya usalama
Mavunde Akabidhi Jengo la kupumzikia Wananchi Hospitali ya Rufaa ya Dodoma
Serikali kufanya mageuzi ya kimtazamo katika nafasi za uongozi kwa wanawake
Waziri Mhagama ametoa Agizo Vituo Vyote Vinavyotoa Huduma za Afya Viweke Wazi Mikataba Kwa Wateja
GRAND BUNGE BONANZA KUFANYIKA JUNI 21 2025 HUKU MGENI RASMI AKITARAJIWA KUWA RAIS SAMIA.
CDE SALUM ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAHAMA MJINI.
KIHENZILE:WIKI YA UTUMISHI WA UMMA NI FURSA MUHIMU KWA WANANCHI
MOI YASEMA WAGONJWA WENGI WANAOWAHUDUMIA WANA MATATIZO SUGU.
PPAA yatoa elimu matumizi ya Moduli Wiki ya Utumishi wa Umma