

Kiongozi wa ACT wazalendo Dorothy Semu ameitaka serikali kuondoa mara moja tozo zote kandamizi zinazozuia biashara ndogo ndogo kuchipua huku akitoa rai kuwa fedha za uchaguzi zisitumike kupora haki na demokrasia kwa wananchi wa nchini.
Kiongozi wa ACT wazalendo Dorothy Semu ameitaka serikali kuondoa mara moja tozo zote kandamizi zinazozuia biashara ndogo ndogo kuchipua huku akitoa rai kuwa fedha za uchaguzi zisitumike kupora haki na demokrasia kwa wananchi wa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo June 21 2025 katika mkutano wa uchambuzi wa bajeti kuu ya serikali jijini Dar es salaam Dorothy amesema serikali inarundika tozo,ushuru,kodi na ada mbalimbali kwa wananchi wenye kipato cha chini huku akiongeza kuwa bajeti haijawapa hauweni umma wa watanzania
Kwa upande wake waziri kivuli wa ACT-wazalendo na Naibu Mwenyekiti ACT wazalendo Isihaka Mchinjita ameeleza kuwa bajeti ya serikali ya 2025-2026 haijatoa nafuu kwa umma wa watanzania bali imeacha maumivu makubwa haswa kwa watu wa hali ya chini hapa nchini kwa sababu haijibu changamoto sugu zinazowakabili wananchi hao.
"licha ya changamoto ya ukosefu wa walimu katika shule za msingi na secondary bajeti haionyeshi mwanga wa kutoa ajira mpya kwa waliimu pia haijatoa kipaumbele kwenye kupunguza changamoto za gharama za matibabu,kupanda kwa gharama na mafuta,dizel na petroli ",Amesema Mchinjita.
Sambamba na hayo ameongeza kuwa deni la taifa limekuwa kubwa na athari ya deni hilo linaangukia kwenye mabega ya wananchi wanyonge na kuongeza kuwa mikopo si njia sahihi ya kuboresha maendeleo ya taifa hili bali serikali ifanye uwekezaj katika miradi mbalimbali itakayonufaisha taifa ukiwemo utekelezaji wa mradi wa gesi na kuongeza ufanisi katika bandari ili kuzikabili changamoto za kiuchumi zinazoikabili nchi
BODI YA MKONGE TANZANIA YATANGAZA FURSA KWA WATANZANIA.
SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUTOKA MWEZI AGOSTI.
DCEA:SERIKALI IMEPUNGUZA KASI YA WALAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.
ULINZI NA USALAMA BAHARINI UMEIMARIKA;TASAC
VITONGOJI VYOTE 64,359 VITAKUWA NA UMEME IFIKAPO 2030
Maiko Salali achukua fomu ya ubunge Jimbo la Mpwapwa
SERIKALI IMEPUNGUZA TOZO KATIKA ZAO LA KAHAWA KUTOKA 17 HADI 5.
Mkoa wa Katavi umeendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM)
UDOM KUJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KUUZA VIMIMINIKA.
AMANZI NA BABU TALE USO KWA USO JIMBONI