

Mapato yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yameongezeka kutoka Shilingi Bilioni 9.55 kwa mwaka 2021/2022 hadi Shilingi Bilioni 25.46 mwaka 2024/2025.
Akizungumza na waandishi wa habari Julai 18 2025, katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anamringi Macha amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2021/22 hadi 2024/25 Mamlaka ya Mapato (TRA) imefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 53.30 sawa na asilimia 108 ya lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 49.44
Aidha Makusanyo ya mapato ya ndani yameongezeka kutoka Shilingi Bilioni 14.232 kwa mwaka 2021/2022 hadi Shilingi Bilioni 18.32 mwaka 2024/2025.
Aidha, katika kipindi cha mwaka 2021/22 hadi 2024/25 Mamlaka za Serikali za Mitaa zimefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 64.09 sawa na asilimia 100 ya lengo la kukusanya Shilingi Bilioni 64.18
"Kupitia ukusanyaji wa mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, pamoja na shughuli nyingine za Maendeleo, Halmashauri zimeendelea kutenga 10% ya mapato yake ili kuwezesha makundi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ambapo kwa kipindi cha miaka Mitano Halmashauri zimefanikiwa kutoa mikopo ya asilimia 10 ya Mapato ya fedha za ndani ambapo jumla ya Shilingi Bilioni 5.13 zimetolewa kwa vikundi 288 vya Wanawake (Bilioni 2.14), vikundi 158 vya Vijana (Bilioni 2.11) na vikundi 84 vya Watu wenye Ulemavu (Milioni 883.34)"Ameongeza
Aidha, Mkoa umeendelea kutekeleza Mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo jumla ya Shilingi Bilioni 3.17 zimetumika katika utoaji wa ruzuku kwa kaya 33,602 zilizo katika mpango wa kunusuru kaya masikini. Mpaka sasa jumla ya Kaya 12,162 zimehitimu kutokana na kuimarika kwa hali zao za kiuchumi.
Aidha, Mkoa umetumia jumla ya Shilingi Bilioni 18.13 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 318 ikiwa miradi 160 ni Miradi ya Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu na Afya na miradi 158 ni ya ukuzaji wa Uchumi wa Kaya na miradi ya ajira za muda.
Mkoa wa Simiyu umeendelea kuwa kinara wa kitaifa katika uzalishaji wa zao la pamba, na sasa umechukua nafasi muhimu kimataifa kupitia kilimo cha pamba hai (organic cotton).
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewezesha mkoa huo kuvuka matarajio kwa kuwekeza katika miundombinu, huduma za ugani na upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima wa pamba.
“Kwa sasa zaidi ya asilimia 60 ya pamba yote nchini huzalishwa hapa Simiyu, na uzalishaji umeongezeka kutoka tani 64,594 mwaka 2020 hadi tani 140,000 mwaka 2024,” amesema Macha.
Ameongeza kuwa Simiyu ni mkoa pekee Tanzania unaolima pamba hai, na uzalishaji wake umeongezeka kutoka tani 10,300 msimu wa 2021/2022 hadi tani 12,285 msimu wa 2022/2023, hali iliyoufanya mkoa huo kushika nafasi ya saba duniani katika uzalishaji wa pamba hai, nyuma ya mataifa kama China, India, Uturuki na Tajikistan.
Aidha, Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU 2018 Ltd) kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), kimefanikiwa kufufua kiwanda cha kuchakata pamba cha Sola Ginnery kilichopo Wilaya ya Maswa kwa gharama ya shilingi bilioni 4.0.
“Kiwanda hiki kimeongeza thamani ya pamba kwa wakulima wetu, kimetoa ajira kwa vijana na kimepunguza gharama za usafirishaji wa mazao ya wakulima,” ameeleza.
Mkoa pia umeendelea kuboresha huduma za ugani na kuwezesha wakulima kupitia maafisa ugani waliopatiwa vifaa vya kisasa, usambazaji wa pembejeo na mikopo midogo ya kilimo kutoka taasisi za fedha.
“Pamba ni zaidi ya zao ni uti wa mgongo wa uchumi wa wakazi wa Simiyu lakini pia tunaishukuru Serikali kwa kuwezesha mapinduzi haya,”
Katika Sekta ya Elimu, kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi mwaka 2025 jumla ya Shilingi Bilioni 119.91 zimetumika kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu mbalimbali ya elimu katika Shule za Msingi, Sekondari.
Hali ya Uchumi ya Mkoa imeendelea kuimarika ambapo Pato la Mkoa limeongezeka kutoka shilingi Trilioni 2.5 mwaka 2020 hadi shilingi Trilioni 3.5 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 42. Vilevile, pato la mtu mmoja mmoja limeongezeka kutoka shilingi 1,096,559 kwa mwaka 2020 hadi shilingi 1,530,577 mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 40.
Mkoa Wa Mara Umezalisha Dhahabu Yenye Uzito Wa Tani 58.90 Sawa na Trillioni 6.90
WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSOMA KATIBA, SHERIA, KANUNI ZA TUME
SALALI:Tunampongeza Rais Samia Kwa Kujumuisha Watu Wenye Ulemavu Dira 2050.
Rais Samia Azindua Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050, Asisitiza Utekelezaji Wa Vitendo Na Upimaji Wa Matokeo
UFUGAJI WA SAMAKI KWA KUTUMIA NJIA YA KISASA UMEONGEZEKA.
IDADI YA WATALII WA NDANI WALIOTEMBELEA MKOA WA TABORA IMEONGEZEKA.
AJIRA ZA MOJA KWA MOJA KATIKA SEKTA YA UTALII ZIMEONGEZEKA.
Uzalishaji wa Madini Umeongezeka kutoka Tani 7.9 Hadi Tani 42.5
DK.NDUMBARO AIPONGEZA OFISI YA MWANDISHI MKUU WA SHERIA.
WAZIRI MKUU MAJALIWA AKABIDHI TUZO YA UMAHIRI KWA MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA NISHATI.