

Katika kipindi mwaka Januari2021 hadi Januari 2025 Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefanikiwa kusajili jumla ya miradi 2,020 ambayo ilikadiriwa kuwekeza kiasi cha mtaji wa Dola za Marekani bilioni 23.67 na kutoa jumla ya ajira 523,891. Kati ya miradi hiyo asilimia 35 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya Wageni na asilimia 23.1 ni ya ubia kati ya Watanzania na Wageni.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Gilead Teri, wakati akizingumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita leo tarehe 27 Februari, 2025, katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma.
Aidha amesema tathmini inaonesha kuwa idadi kubwa ya miradi iliyosajiliwa ipo katika sekta za kipaumbele ambazo ni: Uzalishaji viwandani miradi 538 (45.29%), Usafirishaji miradi 225 (18.94%), Utalii miradi 110 (9.26%), sekta ya ujenzi wa majengo ya biashara miradi 106 (8.92%) Kilimo miradi 106 (8.50%).
Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya Sita kati ya Januari 2021 hadi Januari 2025, TIC imesajili miradi 2,020, ambayo ni ongezeko la asilimia 91 ikilinganishwa na miradi 1,057 iliyosajiliwa katika kipindi cha 2017-2020. Thamani ya mitaji ya miradi hii inakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 23.67, ikiongezeka kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2 katika kipindi cha 2017-2020.
Aidha, miradi hii inatarajiwa kutoa Ajira zilizozalishwa kutokana na usajili wa miradi kumekuwa na ongezeko la Asilimia 284.5 kutoka ajira 136,232 zilizozalishwa kipindi cha miaka minne ya kuanzia mwaka 2017 mpaka 2020 mpaka ajira 523,891 zinazotarajiwa kuzalishwa katika kipindi cha miaka minne ya awamu ya sita kuanzia 2021-2024.
"Kumekuwa na ongezeko la usajili wa miradi kutoka nje linalotokana na juhudi zinazofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuitangaza nchi na kuhamasisha uwekezaji kupitia sera yetu maalum ya mashirikano kupitia Diplomasia ya kiuchumi. Na pia ongezeko la miradi linatokana na ushiriki wa Tanzania katika makongamano mbalimbali nje ya Nchi na maboresho mbalimbali yanayofanywa na Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini.3.1"
Aidha ameongeza kuwa Thamani ya mitaji ya miradi iliyosajiliwa imepanda kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2 hadi bilioni 23.67, ishara ya kuongezeka kwa uaminifu wa wawekezaji kwa serikali ya Awamu ya Sita.
Aidha katika miradi hii, asilimia 34.3 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya wageni, na asilimia 23.1 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni ukilinganisha na miradi iliyosajiliwa katika kipindi cha kuanzia 2017 hadi 2020 ambapo asilimia 27.4 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 44.1 ni ya wageni, na asilimia 28.5 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni.
"Juhudi zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita kushusha kiwango cha chini cha kuruhusu kusajili mradi Kituo cha Uwekezaji ili kupata vivutio kutoka dola za Marekani laki moja mpaka dola 50,000 kimesaidia kuongeza usajili wa miradi ya wawekezaji wa ndani"Amesisitiza
Aidha kituo kimeendelea kuhamasisha uwekezaji wa ndani na nje kwa kuanzisha kampeni mbalimbali za uhamasishaji uwekezaji na kuupa mwaka 2024 kama mwaka wa Uwekezaji.
"Katika kipindi hicho Kituo kimefanikisha upatikanaji wa tuzo mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa TUZO za Kimataifa:za AIM 2024 Mei Taasisi Bora ya Uhamasishaji Uwekezaji Kanda ya Afrika 2024. Desemba 2024 World Association Investment Promotion Agency (WAIPA) kama Taasisi bora inayofanya vizuri katika kutumia mifumo kuhudumia wawekezaji katika nchi zinazoendelea duniani"
Sanjari na hayo hatua nyingine kubwa ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ni mafanikio ya Uanzishwaji wa Jiji la Kilimo la Mkulazi, kwa kipindi kirefu Serikali imefanya juhudi kutafuta wawekezaji ambao wangeweza kuwekeza kwa kiwango ambacho kingeleta manufaa kwa nchi na wananchi wa maeneo ya Mkulazi ili kupunguza uagizaji kutoka nje ya nchi bidhaa za kilimo hususani Sukari, nafaka, sukari na mazao mbalimbali yatakayoingiza fedha za kigeni baada ya mauzo ya nje.
"Hivyo basi , kupitia mchakato wa wazi, TIC kwa kushirikiana na Taasisi na Idara mbalimbali za Serikali ilifanya tathmini ya maombi ya Makampuni yaliyoonesha nia ya kuendeleza shamba la Mkulazi na Makampuni matatu yalijitokeza na kazi ya uendelezaji wa miradi inaendelea. Miradi hiyo inatarajia kuleta mitaji ya dola za kimarekani 575 milioni kuzalisha Ajira 10,000 za moja kwa moja"Ameongeza
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.
UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.
MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.
UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.
MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.
WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.