NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.

NCAA, kwa kushirikiana na vikosi maalum na vyombo vya usalama, imefanikiwa kudhibiti ujangili wa wanyamapori ndani na nje ya Hifadhi ya Ngorongoro na Pori la Akiba la Pololeti.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
10 Mar 2025
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.


Hayo yameelezwa na Dkt.Elirehema J.Doriye Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya hifadhi Eneo la Ngorongoro (NCAA) wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya Sita kuelezea mafanikio na mwelekeo wa hifadhi hiyo Machi 10 2025,katika Ofisi za Idara ya Habari MAELEZO, jijini Dodoma.


Aidha amesema Matukio ya ujangili wa tembo yamepungua kutoka 25 mwaka 2020/2021 hadi tukio moja tu mwaka 2022/2023, na hakuna tukio lolote mwaka 2024 ambapo Mamlaka imekamata watuhumiwa 207 wa ujangili, ambapo 175 wamefikishwa mahakamani.

"Mitandao ya ujangili inayotumia sumu na silaha za jadi imevunjwa katika maeneo mbalimbali,Mafanikio haya yanatokana na ushirikiano madhubuti na matumizi ya teknolojia za kisasa katika kulinda wanyamapori"

Aidha Mamlaka imeendelea kutunza hadhi zake za kimataifa kutoka UNESSCO kama eneo lenye urithi mchanganyiko, Biosphere Reserve na Global Geopark.

"Eneo hili linaendelea kuwa moja ya maajabu saba ya asili barani Afrika, likiwa na miamba na sura za nchi zinazoelezea historia ya dunia na uumbaji wake"

Aidha NCAA imeendelea kudhibiti mimea vamizi  zaidi ya hekta 5,207.5 ndani ya hifadhi ambapo hatua hii imeboresha uhifadhi wa wanyamapori na ikolojia yao,Mfumo wa ufuatiliaji wa wanyamapori umeimarishwa ambapo faru 29 wamewekewa alama za masikio na vinasa mawimbi kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wao na kuimarisha ulinzi.

Aidha Hifadhi ya Ngorongoro ni eneo la kipekee duniani kwani lina hadhi tatu zinazotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), ambazo ni:Man and Biosphere Reserve (Hifadhi ya Binadamu na Baiolojia), hadhi inayothibitisha umuhimu wa uhifadhi endelevu unaojumuisha binadamu na mazingira ya asili,Mixed World Heritage Site (Urithi wa Dunia Mchanganyiko), inayotambua thamani ya kipekee ya maliasili na urithi wa kiutamaduni uliopo ndani ya eneo la hifadhi,Ngorongoro Lengai UNESCO Global Geopark (Hifadhi ya Jiolojia ya Dunia), ambayo inahusisha mandhari ya kipekee ya kijiolojia, milima, volkano, na mabonde ambayo yanaelezea historia ya mabadiliko ya dunia.

Aidha Mamlaka imejenga vituo viwili vya askari katika Wilaya za Korogwe na Same kwa ajili ya kusaidia Serikali kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo ya wananchi.

Sanjari na hayo Ili kudhibiti migogoro ya ardhi na uvamizi wa maeneo ya hifadhi, NCAA imejenga vigingi 110 katika mipaka ya hifadhi kwa lengo la kuimarisha utambuzi wa maeneo yaliyohifadhiwa ambapo Mamlaka imeotesha na kugawa miche ya miti 1,150,188 katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha Idadi ya faru weusi imeongezeka kwa 40% kutoka mwaka 2020 hadi 2024, kutokana na juhudi madhubuti za uhifadhi huku Idadi ya simba ndani ya hifadhi imefikia takriban 188 na Idadi ya tembo imeongezeka kutoka 800 mwaka 2020 hadi makadirio ya 1,300 mwaka 2024.

Aidha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeimarisha ulinzi wa rasilimali, hali iliyosaidia kudhibiti ujangili na kurejesha mfumo wa kiikolojia wa Serengeti-Masai Mara. Hatua hizi zimechochea urejeo wa uoto wa asili na malisho ya wanyamapori.

"Matukio ya ujangili wa tembo yamepungua kutoka 25 mwaka 2020 hadi sifuri mwaka 2024 katika Ngorongoro na Pololeti. Kwa kushirikiana na vikosi vya usalama, NCAA imefanikiwa kukamata watuhumiwa 207 wa ujangili, huku mitandao ya ujangili kwa sumu na silaha za jadi ikidhibitiwa"

Aidha, NCAA imetekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuhakikisha taasisi zote za umma na binafsi zinasajiliwa na kutekeleza Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022. NCAA imesajiliwa kama msindikaji na mdhibiti wa data kwa mujibu wa Kifungu cha 14(2) cha Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Sura ya 44 ya mwaka 2022, na imeshapata cheti cha usajili kuthibitisha utekelezaji wa sheria hii

OPARESHENI YA KUWADHIBITI FISI SIMIYU YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA

OPARESHENI YA KUWADHIBITI FISI SIMIYU YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA

WATANGAZAJI WAASWA KUACHA KUKIFUBAZA KISWAHILI.

WATANGAZAJI WAASWA KUACHA KUKIFUBAZA KISWAHILI.

Serikali imewahimiza wananchi kutumia msimu wa Sikukuu na likizo kutembelea Vivutio vya Utalii.

Serikali imewahimiza wananchi kutumia msimu wa Sikukuu na likizo kutembelea Vivutio vya Utalii.

ZOEZI LA KULIPA FIDIA WANANCHI NGOMBO LINAKWENDA VIZURI : DC MALINYI

ZOEZI LA KULIPA FIDIA WANANCHI NGOMBO LINAKWENDA VIZURI : DC MALINYI

HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO

HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO