OPARESHENI YA KUWADHIBITI FISI SIMIYU YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA | The Dodoma Post
The Dodoma Post Utalii

OPARESHENI YA KUWADHIBITI FISI SIMIYU YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA

Oparesheni maalumu ya kuwadhibiti wanyamapori wakali na waharibifu aina ya fisi waliokuwa wanaleta taharuki na madhara Kwa jamii inayoendelea Mkoani Simiyu imeonesha mafanikio makubwa baada ya fisi 16 kuvunwa ikiwa ni hatua muhimu iliyochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuhakikisha usalama na utulivu Kwa wananchi vinarejea.

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
20 Feb 2025
OPARESHENI YA KUWADHIBITI FISI SIMIYU YAONESHA MAFANIKIO MAKUBWA

* Zaidi ya Fisi 16 wavunwa.

Oparesheni maalumu ya kuwadhibiti wanyamapori wakali na waharibifu aina ya fisi waliokuwa wanaleta taharuki na madhara Kwa jamii inayoendelea Mkoani Simiyu imeonesha mafanikio makubwa baada ya fisi 16 kuvunwa ikiwa ni hatua muhimu iliyochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ya kuhakikisha usalama na utulivu Kwa wananchi vinarejea.

Hayo yamesemwa leo Februari 19, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi alipokuwa akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

Kihongosi amesema kufuatia changamoto hiyo,  Serikali ilichukua jukumu kubwa la kuhakikisha inalinda wananchi wake ikiwemo kuanzisha oparesheni maalumu inayohusisha Jeshi la Uhifadhi Kwa Taasisi za TAWA, TANAPA na TFS Kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na wananchi, oparesheni inayotajwa kuanza  Januari 25, 2025.

"Tarehe 20/12/2024 baada ya fisi kuvamia wananchi Serikali ilichukua hatua kubwa ya kushirikisha vyombo vyake (TAWA na Jeshi la Polisi) na kuanza Oparesheni, lakini ilipofika tarehe 25/01/2025 oparesheni ya mkoa mzima ilifanyika Kwa ukubwa kuhakikisha inakabiliana na fisi wote waliokuwa wanasumbua wananchi" amesema Kihongosi 

"Na Kwa taarifa njema ni kwamba tangu kuanza Kwa oparesheni hii vyombo vyetu vimeweza kudhibiti na kuua fisi 16 na ndio maana kwasasa mnaweza kuona hali imetulia" ameongeza Mkuu huyo wa mkoa wa Simiyu.

Aidha Kihongosi ameendelea kuwatoa hofu wananchi wa mkoa huo akisisitiza kuwa hali ni shwari na kuwataka waendelee na shughuli zao kama kawaida huku akikemea vikali imani za kishirikina kuhusiana na mnyamapori aina ya fisi kwa baadhi ya wakazi wa Simiyu na kuwataka wote wanaofuga wanyamapori pori hao kuacha mara moja kwani ni kosa kisheria kumiliki nyara za Serikali bila Kibali.

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja amewaomba wananchi wa Mkoa wa Simiyu hususani wilaya ya Itilima kuacha tabia ya kutembea  nyakati za usiku na alfajiri kwani ni nyakati ambazo wanyama fisi huwa katika mawindo yao.

Vilevile amewasisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Maofisa wa Jeshi la Uhifadhi waliopo uwandani ili kuongeza ufanisi wa zoezi hilo huku akiwahakikishia  kuwa Serikali imedhamiria kulinda wananchi wake na kwamba Askari wapo uwandani wanafanya Kazi usiku na mchana kuwahakikishia usalama wao.

Nao, wananchi wa Simiyu hususani wilaya ya Itilima wameshukuru Kwa juhudi zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na changamoto hiyo, wakisema kuwa hatua hiyo imeweza kuwarejeshea matumaini, utulivu na amani.

"Kwakweli tulikuwa tunasumbuliwa sana na haya mafisi ambayo yalikuwa yanauma watu, baada ya Serikali kusikia ikaweka ulinzi, kwakweli imetufanyia vizuri sana mpaka leo hatujawasikia tena tangu Askari waanze kuwashambulia hao fisi, mpaka leo hii tuna utulivu sana kwakweli tunashukuru sana"   amesema Mozo Mabula  mkazi wa Kijiji cha Mwamunhu kilichopo wilaya ya Itilima.

NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.

NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.

WATANGAZAJI WAASWA KUACHA KUKIFUBAZA KISWAHILI.

WATANGAZAJI WAASWA KUACHA KUKIFUBAZA KISWAHILI.

Serikali imewahimiza wananchi kutumia msimu wa Sikukuu na likizo kutembelea Vivutio vya Utalii.

Serikali imewahimiza wananchi kutumia msimu wa Sikukuu na likizo kutembelea Vivutio vya Utalii.

ZOEZI LA KULIPA FIDIA WANANCHI NGOMBO LINAKWENDA VIZURI : DC MALINYI

ZOEZI LA KULIPA FIDIA WANANCHI NGOMBO LINAKWENDA VIZURI : DC MALINYI

HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO

HARUSI YA KIHISTORIA YAFUNGWA KRETA YA NGORONGORO