

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa serikali za mitaa kote nchini kujiepusha kuwa vyanzo vya migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao, akiwataka kuwa sehemu ya masuluhisho ya migogoro hiyo.
Wakati wa Mkutano mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za mitaa Tanzania Alat Ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma Machi 11, 2025, Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi wa mkutano huo ameitaja migogoro ya ardhi kama Donda sugu kwenye jamii, akiitaja kama chanzo cha uhasama na mauaji kwenye ngazi ya jamii.
Katika hatua nyingine Rais Samia pia amewataka watendaji wa serikali za mitaa kuendelea kusimamia watumishi na watendaji wa mamlaka zao katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi kwa kuwapokea na kuwasikiliza kwa busara sambamba na kuimarisha mifumo ya ushughulikiaji wa kero za wananchi kwa wakati.
Rais Samia pia katika hotuba yake amesisitiza kuhusu kuoanisha mipango ya ngazi ya Halmashauri na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa pamoja na kusisitiza juhudi zaidi katika kubuni na kuimarisha vyanzo vya mapato na kujiepusha na migogoro kati yao na wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali na badala yake wakuze na kuimarisha mahusiano mazuri kati yao.
Rais Samia amesema katika kuelekea harakati za uchaguzi, endapo kuna wakurugenzi na wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya wanaotaka kuingia majimboni watoe taarifa mapema ili waanze kuandaliwa waliopo chini yao kwa lengo la kuwapandisha vyeo badala ya wateule hao kuondoka na kusababisha teuzi kuwa ngumu.
"Kwa sasa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu kama kuna wakurugenzi,wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaotaka kwenda kugombea watoe nafasi mapema ili tuanze kuwatengeneza waliopo chini yao kushika nafasi hizo.
“Kuna wakati unakuta watu wote wanaondoka kwenda kuchukua fomu na kuziacha ofisi hazina watendaji kutokana na hali hiyo inapelekea kuteua watu ambao hawana uzoefu jambo ambalo siyo sahihi.
“Kama mtu anataka kwenda kuchukua fomu ni lazima kujipima na kutoa taarifa iwapo haukutoa taarifa unaweza kujikuta unakosa yote maana unaweza kukosa huko na huku ukakuta nafasi yako imejazwa lakini kama utatoa taarifa na ulikuwa mtendaji mzuri unaweza kufikiriwa.
“Tunataka watu wanaokwenda kugombea ni watu ambao tayari wamejipanga na wana uwezo wa kuendesha gurudumu la maendeleo na siyo watu ambao hawajajiaandaa,”amesema.
Katika hatua nyingine amezitaka halmashauri kuhakikisha inasimamia mapato yanayokusanywa katika halmashauri zao kwa lengo la kufanikisha maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
DKT. BITEKO AKUTANA NA MTENDAJI MKUU WA CLIMATE INVESTMENT FUNDS
KAMATI ya Bunge ya miundombinu yaridhishwa na kasi ujenzi daraja la pangani
MIKOA 16 kunufaika na Nishati ya Jotoardhi
MASAA YA Upatikanaji wa Huduma ya Maji Yameongezeka Kutoka saa 16 hadi saa 22
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wadau wa kemikali
Hatua Kali Za Kisheria Kuchukuliwa Kwa Watakaoghushi Cheti Cha Kuhitimu Mafunzo ya JKT.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.
DAWASA Imeendelea na Utekelezaji wa Miradi Zaidi ya 25 Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 987.6.