DAWASA Imeendelea na Utekelezaji wa Miradi Zaidi ya 25 Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 987.6. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

DAWASA Imeendelea na Utekelezaji wa Miradi Zaidi ya 25 Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 987.6.

Katika kipindi cha kuanzia Julai 2021, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea na utekelezaji wa miradi zaidi ya ishirini na tano (25) yenye thamani ya fedha za Kitanzania Shilingi bilioni 987.6. ambapo kati ya hizo Bilioni 987.6, ni Miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 754.7 bado ipo katika hatua mbalimbali za,Miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 232.9 imekamilika na inatoahuduma kwa wananchi.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
12 Mar 2025
DAWASA Imeendelea na Utekelezaji wa Miradi Zaidi ya 25 Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 987.6.

Hayo yameelezwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita  Machi 11, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.

Aidha miradi iliyopo katika mipango ya muda mfupi na mrefu yenye thamani ya Shilingi Trilioni3.1 imebuniwa na iko katika hatua mbalimbali za maandalizi ambapo Fedha hizo zina jumuisha gharama za usanifu,ujenzi,upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya uzalishaji,usafirishaji na usambazaji wa majisafi,pamoja na ujenzi,upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya ukusanyaji,usafirishaji,upokeaji na uchakataji wa majitaka.

Aidha Miradi hiyo inatekelezwa kwa kutumia fedha za makusanyo ya DAWASA,Serikali kuwa na mikopo ya masharti nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo,wakiwemo Benki ya Dunia,Serikali ya Korea Kusini(kupitia Benki ya Exim ya Korea)na Serikali ya India(kupitia Benki ya Exim ya India).

Aidha Uwezo wa uzalishaji maji umeongezeka kutoka lita 520,000,000/siku mpaka lita 534,600,000/siku sawa na ongezeko la lita14,600,000/siku huku Uwezo wa kuhifadhi maji umeongezeka kutoka lita153,649,000 hadi lita 198,965,000 sawa na ongezeko la lita 45,316,000

"Mtandao wa usafirishaji na usambazaji maji umeongezeka kutoka kilomita4,690.7 hadi kilomita7,206 sawa na ongezeko la kilomita 2,513.4,Mtandao wa majitaka umeongezeka kutoka kilo mita450 hadi kilomita 519.4 sawa na ongezeko la kilomita 69.4"

Aidha Idadi ya maunganisho ya wateja wamajisafi imeongezeka kutoka 343,019 hadi 455,720 sawa na ongezeko la wateja 112,701 ambapo kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma ya majisafi kutoka wastani wa asilimia 89 hadi asilimia 93 na huduma ya usafi wa mazingira kutoka asilimia 25 hadi asilimia 45.

"DAWASA IMEFANIKIWA kuanza kwa utekelezaji wa bwawa la Kidunda–Mkataba wenye thamani ya Shilingi bilioni 335.9,hadi sasa Shilingi bilioni 85.4 zimetolewa na mradi umefikia asilimia 28 pamoja na kutolewa kwa kibali cha kuanza maandalizi ya mradi mkubwa wa kutoa maji kutoka Mto Rufiji ambapo utatosheleza mahitaji mwisho(detaileddesign)pamoja na kuandaa nyaraka za maji hadi mwaka 2050,utekelezaji wakuandaa michoro ya manunuzi(biddingdocuments)umefikia asilimia 89.

Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.

Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.

RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya  Migogoro ya Ardhi Nchini.

RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.

JAJI WARIOBA: NAPONGEZA CCM KWA HATUA ZAKE DHIDI YA RUSHWA.

JAJI WARIOBA: NAPONGEZA CCM KWA HATUA ZAKE DHIDI YA RUSHWA.

WATENDAJI UBORESHAJI WA DAFTARI MOROGORO, TANGA WAHIMIZWA KUZINGATIA SHERIA.

WATENDAJI UBORESHAJI WA DAFTARI MOROGORO, TANGA WAHIMIZWA KUZINGATIA SHERIA.

DKT.NCHIMBI AKEMEA KITENDO CHA MAKADA CCM KUTENGENEZA MATUKIO BINAFSI KWA KIVULI CHA CCM NA KUWALIPA POSHO WANACHAMA.

DKT.NCHIMBI AKEMEA KITENDO CHA MAKADA CCM KUTENGENEZA MATUKIO BINAFSI KWA KIVULI CHA CCM NA KUWALIPA POSHO WANACHAMA.