

Watendaji wa uboreshaji wa Daftari; la Kudumu la Wapiga Kura wameaswa kutekeleza majukumu waliyopewa kwa kuzingatia sheria, kanuni, maelekezo na miongozo itakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Watendaji wa uboreshaji wa Daftari; la Kudumu la Wapiga Kura wameaswa kutekeleza majukumu waliyopewa kwa kuzingatia sheria, kanuni, maelekezo na
miongozo itakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Balozi Omari Ramadhan Mapuri wakati akifunga mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa daftari mkoani Morogoro leo Februari 19, 2025.
“Mnapaswa kutekeleza majukumu mliyopewa kwa kuzingatia sheria, kanuni,maelekezo na miongozo itakayotolewa na Tume,” amewaasa watendaji hao ambao wamehudhuria mafunzo ya siku mbili.
Balozi Mapuri ametoa wito kwa watendaji hao kuendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia maelekezo yote waliyopewa ili kuongeza uelewa zaidi
kuhusu wajibu na majukumu yao wakati wa kutekeleza zoezi lililopo mbele yao.
Akifunga mafunzo kama hayo mkoani Tanga, Mjumbe wa Tume ambaye pia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari amewataka watendaji hao kusoma katiba na
sheria ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
“Someni kwa makini Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya Uchaguzi, Kanuni za uboreshaji, Maelekezo na Miongozo yote inayotolewa na Tume
ili kazi yenu ifanyike kwa unadhifu na haki,” amesema.
Jaji Asina amewakumbusha watendaji hao juu ya wajibu wao wa kuhamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba
itakayowawezesha kushiriki katika kuchagua viongozi wao kwenye uchaguzi mkuu utakoafanyika mwaka huu.
Uboreshaji wa Daftari utafanyika mkoani Morogoro na kwenye Mkoa wa Tanga katika Halmashauri za Wilaya ya
Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga kwa siku saba kuanzia tarehe 01 hadi 07 Machi, 2025 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa
saa 12:00 jioni.
Kylian Mbappé: Mapambano ya Kifundo cha Mguu na Tumaini la Ushindi
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
DAWASA Imeendelea na Utekelezaji wa Miradi Zaidi ya 25 Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 987.6.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.
MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.
WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.