Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Tanzania

Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.

Vituo 94 vimepewa mikopo na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi ambapo mwelekeo wa NHIF ni kutumia TEHAMA kuendelea kuimarisha huduma zake kwa wananchi ili kurahisisha utoaji wa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
10 Mar 2025
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dkt. Irene Isaka wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Mfuko huo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita Machi 10, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.

Aidha amesema NHIF inakwenda kusajili makundi maalumu kama wakulima, wajasiriamali na mengine.

"Tunawasihi wananchi kuendelea kujitokeza kwa ajili ya kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, msisubiri hadi mnapokuwa wagonjwa ndipo mshughulikie kupata Bima ya Afya" Nasisitiza kuondoa dhana ya kwamba Bima ya Afya ni uchuro.

"Tumekubaliana na UTPC kuwasajili waandishi wa habari wote ambao ni wakujitegemea ili waweze kuwa wanufaika ili kupata huduma ya Bima ya Afya"

Aidha amesema Kutakuwa na Mfuko wa kuhudumia kaya masikini kupitia NHIF, baada ya utambuzi kufanywa na Mamlaka za utambuzi kama TASAF na TAMISEMI vilevile mfuko umeongeza vituo vya kutolea huduma kufikia 10,04,00.

Aidha Shilingi trilioni 2.29  zimelipwa kwa watoa huduma waliohudumia wanachama wa NHIF ambapo Bilioni 91 zimelipwa kwa watoa huduma waliohudumia wanachama wa NHIF ambao ni wastaafu.

Aidha Bilioni 22 zimeokolewa kutokana na usimamizi madhubuti wa mfuko wa NHIF, fedha hii ilikuwa inapotea kutokana na udanganyifu wa baadhi ya wanachama

"Watumishi 36 wa vituo vya kutolea huduma wamechukuliwa hatua kwa kufanya udanganyifu kwenye mfuko"

Aidha Madai ya watoa huduma za afya yanafanyika ndani ya siku 60 ikilinganishwa na siku 120 za awali kabla ya uwepo wa mifumo,katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita wamesajili wanachama milioni 2.2

Sanjari na hayo Ukusanyaji wa michango umefikia trilioni 2.3 kwa sasa kutokana na maboresho yaliyofanyika katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita.

"Ulipaji malipo ya watoa huduma unafanyika kwa wakati kwa kuzingatia huduma mpya za afya zinazotolewa"

"Tumefanikiwa kuimarisha mifumo ya TEHAMA katika shughuli za mfuko ili kuimarisha utendaji na tija"Ameongeza

Aidha Mwananchi anaweza kujisajili ili kujiunga na mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya kwa kutumia mfumo wa TEHAMA ambapo Mwanachama anaweza kupata huduma za afya kupitia namba yake ya NIDA si lazima awe na kitambulisho cha NIHF.

"NHF ina mfumo wa kutambua utendaji wa watumishi wake kutumia TEHAMA, Tumeunganisha mifumo yetu na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo NIDA, RITA, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), TIRA,TRA na Wizara ya Afya"

" Mfumo madai ya watoa huduma wetu unachakata madai yote na unauwezo wa kufanya uchambuzi wa taarifa zilizowasilishwa za madai na kuondoa udanganyifu"

Aidha Malipo ya watoa huduma yanafanyika kwa wakati kwa sababu ya uwepo wa mifumo ya TEHAMA.

UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.

UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.

KIWANGO Cha Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali Kimepanda Kutoka Shilingi Bilioni 624.61 hadi Bilioni 753.82

KIWANGO Cha Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali Kimepanda Kutoka Shilingi Bilioni 624.61 hadi Bilioni 753.82

JUMLA YA MIRADI 2,020 IMEFANIKIWA KUSAJILIWA NA TIC.

JUMLA YA MIRADI 2,020 IMEFANIKIWA KUSAJILIWA NA TIC.

BoT: Tunatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga uchumi wa nchi

BoT: Tunatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga uchumi wa nchi