GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.

Gharama ya kupandikiza mimba ni milioni 14 Hospitali ya Taifa Muhimbili hii ni kutokana na gharama ya huduma hiyo ambayo ina hatua nyingi na imewapunguzia gharama watanzania ya kwenda nje ya nchi ambapo gharama inakuwa kubwa zaidi ya iliyotajwa

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
06 Mar 2025
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Rachel Mhaville wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi, kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita tarehe 6 Machi, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma.


Aidha amesema Hospitali imefanikiwa kuanzisha matibabu ya magonjwa ya ngozi kwa njia ya tiba mwanga (phototherapy) na tiba laser ikiwa ni hospitali pekee nchini inayotoa huduma hii ambapo huduma hii imekuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wenye matatizo ya vitiligo na saratani za ngozi ambapo wastani wa wagonjwa 10 hadi 15 wanahudumiwa kwa wiki. (tatooo) 3.13

Aidha Hospitali imefanikiwa kuanzisha kliniki kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 18 mpaka 26 ambayo inaendeshwa kwa pamoja na timu ya madaktari bingwa wa kisukari wa watoto na watu wazima ili kuwajenga vijana hao kiafya na kisaikolojia katika kuishi na ugonjwa wa kisukari aina ya kwanza.

Aidha ameongeza kuwa Serikali imewezesha kununua mashine ya kisasa kabisa inayowezesha uchunguzi wa magonjwa ya mifupa ya taya pamoja na CT scan ya uso na kichwa kusaidia kupanga upandikizaji wa vipandikizi vya meno ambapo tangu kununuliwa mwishoni mwa mwaka 2024 tayari wagonjwa 2,251 wamenufaika.

Aidha Hospitali imefanikiwa pia kuanzisha huduma hiyo nchini na yenye watalaam wabobezi wa kutoa huduma za upimaji na matibabu ya mzio (allergy)ambapo jumla ya wananchi 470 wametibiwa tangu kuanzishwa kwa huduma hii mwaka jana 2023 ambapo MNH ni hospitali ya kwanza kutoa huduma hii kwa kiwango cha ubobezi hapa nchini.

"Tulianzisha huduma ya kuondoa sehemu yenye ugonjwa kwenye taya kisha kuvuna sehemu ya mbavu pamoja na mfupa wa nyonga kwa kutumia vipandikizi maalum kuunda mfupa wa taya jipya la chini ili kumrejeshea mgonjwa muonekano mzuri lakini pia huweza kupandikizwa meno na kumrejeshea mgonjwa uwezo wa kula tena"

" Tumeanzisha matibabu ya kuziba mapengo ambapo mzizi bandia hupandikizwa kwenye taya, kisha kuwekewa meno juu yake yanayogandishwa na kutumika kama sehemu ya meno yake ya kuzaliwa nayo"Ameongeza

Sanjari na hayo Hospitali iliendelea kuhakikisha dawa na vitendanishi vinapatikana muda wote ili kuondoa usumbufu kwa wagonjwa ambapo kwa sasa kiwango cha dawa kinapatikana ndani ya Hospitali kwa asimilia 98 zenye thamani ya TZS. 134.7.  

Aidha Hospitali Katika kuimarisha mazingira na miundombinu, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha mwonekano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia lango kuu ili kuwa na unadhifu pamoja sura halisi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa nje na ndani. Sambamba na hilo, kwa sasa waenda kwa miguu wametengewa eneo la kuingia na kutoka ili kuongeza usalama wao dhidi ya vyombo vya moto.  

Aidha Hospitali ya Taifa Muhimbili kama taasisi ya Serikali imeendelea kutekeleza Sera na Miongozo mbalimbali ya Wizara ikiwamo utoaji huduma za misamaha kwa wagonjwa wasio na uwezo wa kuchangia.  Katika kipindi hicho, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa huduma kwa njia ya msamaha hospitalini hapo zenye thamani ya TZS. 80.6 Bil ambapo iligusa maeneo ya vipimo vya maabara, radiolojia, dawa, malazi huduma ya ICU nakadhalika.

Aidha Hospitali imeimarisha hali ya upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi kwa kuongeza hali ya uwajibikaji wa wafanyakazi katika maeneo yote ya kutoa huduma kuanzia kwa Wakurugenzi, Wakuu wa Idara, Madaktari Bingwa hadi Wahudumu wa aina zote KWAKUWA MTEJA NI MFALME.

MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.

MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.

WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.

WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.

RIKA LINALOTAKA KUPANDIKIZWA MIMBA NI KUANZIA MIAKA 35 HADI 50.

RIKA LINALOTAKA KUPANDIKIZWA MIMBA NI KUANZIA MIAKA 35 HADI 50.

Vikundi 21 kunufaika na Mradi wa Tuinuke Pamoja Kukuza Usawa wa Kijinsia Kondoa, Chemba

Vikundi 21 kunufaika na Mradi wa Tuinuke Pamoja Kukuza Usawa wa Kijinsia Kondoa, Chemba

JAMII IMEHAMASISHWA KUZINGATIA MTINDO BORA WA MAISHA KWA KUFANYA MAZOEZI ILI KUJIEPUSHA NA MAGONJWA YA MOYO

JAMII IMEHAMASISHWA KUZINGATIA MTINDO BORA WA MAISHA KWA KUFANYA MAZOEZI ILI KUJIEPUSHA NA MAGONJWA YA MOYO