

Jumla ya vikundi 21 vinavyotoka Kondoa na Chemba kwenye Halmashauri tatu za Kondoa Dc, Kondoa TC na Chemba vinatarajia kunufaika na Mradi wa Tuinuke Pamoja, unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya TGNP, Agha Khan Foundation, na ufadhili wa Ubalozi wa Ireland hapa Tanzania, unalenga kuleta usawa wa kijinsia .
Meneja Mradi wa Tuinuke Pamoja
Nestor Mhando,ameeleza hayo February 28,2025 Wilayani Kondoa kwenye mafunzo ya kuvijengea uwezo vikundi hivyo ambapo ameeleza kuwa kila Hamlashauri imetoa vikundi 7 ambavyo vyote kwa pamoja vinatekeleza bunifu mbalimbali zenye kuchangia kuleta Usawa wa kijinsia katika maeneo yao.
Ameeleza kuwa Mradi huo wa miaka mitatu, ulioanza rasmi mwezi Julai 2024, unashirikisha vikundi vya kijamii kutoka Kata za Kondoa na Chemba, mkoani Dodoma ambapo vikundi hivyo vina nafasi muhimu katika kubuni suluhisho la kudumu kwa changamoto za kijinsia na kijamii zinazoikumba jamii .
Licha ya hayo ameeleza kuwa lengo kuu la mradi huo ni kuimarisha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake kushiriki kwa usawa katika nafasi mbalimbali za kijamii.
"Katika kutekeleza malengo haya, hatua muhimu zimechukuliwa kama vile kutambua vikundi vya kijamii vinavyofanya kazi moja kwa moja na wananchi ambapo jukumu letu ni kuvipatia mafunzo na msaada wa kifedha ili kujenga uwezo wao katika nyanja mbalimbali, hususan usawa wa kijinsia, "amefafanua Meneja Mradi huo
Ili kutekeleza mawazo bunifu ambayo yatakuwa na mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko ya kijinsia katika jamii, Meneja huyo ametaja baadhi ya bunifu zinazotekelezwa na vikundi hivyo kuwa ni pamoja na elimu ya afya kwa wanafunzi mashuleni, kuimarisha upatikanaji wa haki sawa kwa watoto, kupinga ukatili, na kuelimisha jamii kuhusu haki za kijinsia na afya.
Mhando amesema vikundi hivi ni muhimu kwa kuwa viko katika nafasi nzuri ya kutambua changamoto zinazoikumba jamii na kuzitafutia suluhisho.
"Kupitia juhudi hizi, wanawake na watoto wa kike wataweza kujiinua kiuchumi na kijamii, na hatimaye kuwa na usawa na haki katika jamii, " ameeleza
Mhando anasema kuwa mafanikio ya mradi huu ni mwanzo wa mabadiliko makubwa katika jamii, ambapo usawa wa kijinsia utaimarika na wanawake na watoto wa kike watawezeshwa kufikia malengo yao.
"Pamoja na juhudi hizi tunashirikiana na wadau mbalimbali wa mashirika yanahusiana na haki za wanawake na Asasi za kiraia katika mchakato mzima wa kufanya maandalizi ya nyenzo mbalimbali kwa ajili ya kujengea uwezo hivi vikundi ambavyo moja kwa moja vitaenda kutekeleza kwenye jamii,
Hadi sasa tupo kwenye hatua za mwisho za kuwajengea uwezo na kuimarishana ikiwa ni pamoja na kusaini mikataba kwa ajili ya utekelezaji wa maeneo husika, "amefafanua.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Hadija Mohammed Huseni kutoka kijiji cha Kidoka, Wilaya ya Chemba, ambaye ni mjasiriamali katika ufugaji wa kuku, anasema kuwa mafunzo yaliyotolewa yamewasaidia kuelewa haki za wanawake na kuondokana na mfumo dume.
Amesema kuwa wanajivunia kuwa na uelewa wa haki za walemavu na wajane, na kwamba kupitia mafunzo hayo wataelimisha jamii kuhusu namna ya kupambana na unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.
Tuinuke Pamoja ni mradi wa kipekee ambao umeleta matumaini kwa wanawake na watoto wa kike, na utaendelea kuwa na mchango mkubwa katika kukuza haki za kijinsia na kuboresha maisha ya jamii katika maeneo yanayoshirikishwa.
Matarajio ni kwamba jitihada hizi zitaendelea kuchochea mabadiliko ya kijamii ambayo yatadumu kwa vizazi vijavyo.
Ametaja baadhi ya bunifu zilizopo kwenye vikundi hivyo 21 kuwa ni pamoja na elimu ya afya wa wanafunzi mashuleni, kulenga kuimarisha upatikanaji wa haki sawa kwa watoto,kupinga ukatili, bunifu za elimu ya kijinsia na Afya na nyinginezo.
Kupia bunifu hizo inatujenga na kututia moyo Sisi Kama wadau kuona bunifu zote hizo zitachangia kufikia Usawa wa kijinsia na kuwezesha mwanamke na mtoto wa kike kujiinua na kujitegemea.
Kwa upande wa baadhi ya wadau wa vikundi walioshiriki mafunzo hayo wameeleza kufurahishwa na mafunzo hayo na kueleza kuwa yatawajenga kijamii.
Hadija Mohammed Husen kutoka kijiji cha Kidoka wikaya ya Chemba amesema kikundi chake kinajihusisha na ugugaji wa kuku ambao wamekuja na ubunifu wa unyanyasaji wa kijinsia ,ukatili na kujifunza uchumi.
Amesema wanepata manufaa kwenye mafunzo hayo ambayo yatawanufaisha kujua haki za wanawake katika kujiinua kiuchumi na kuondokana na mfumo dume kwenye jamii
Kylian Mbappé: Mapambano ya Kifundo cha Mguu na Tumaini la Ushindi
Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.
RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.
DAWASA Imeendelea na Utekelezaji wa Miradi Zaidi ya 25 Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 987.6.
NCAA IMEFANIKIWA Kudhibiti Ujangili wa Wanyamapori Ndani na Nje ya Hifadhi ya Ngorongoro.
UPOTEVU Wa Maji Kwa Mwaka 2021 Ulikuwa Wastani wa Asilimia 64.
MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.
GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.
WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.
Vituo 94 vimepewa mikopo na NHIF kwa ajili ya kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.