WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.

Wananchi wa Nne kutoka Mkoa wa Tanga wamefika jijini Dodoma kuwakilisha wananchi zaidi 1000 katika kijiji cha Bondo Wilayani Kilindi Mkoani Tanga ili kuonana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kufikisha kilio chao kwa kile wanachodai kuchomewa moto nyumba zao na mazao yao kuharibiwa kwa madai ya kuwa wanaishi katika msitu wa hifadhi unamilikiwa na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS)

Mwandishi Wetu
By Mwandishi Wetu
05 Mar 2025
WANANCHI WAILILIA SERIKALI,WAFUKUZWA KWENYE MAENEO YAO.

Wananchi hao walifika Jijini hapa Machi Mosi,2025 na kuzungumza na waandishi wa habari kabla ya safari yao ya kwenda kumuona Waziri Mkuu.

Daniel Naoki mmoja ya wananchi hao waliofika Dodoma aliwaambia waandishi wa habari kuwa hali yao ni mbaya kwani wamejikuta hawana makazi baada ya wanachodai nyumba zao kuchomwa moto na mazao yao kuharibiwa kwa madai kuwa walikuwa wakiishi katika eneo la hifadhi linalomilikiwa na TFS.

"Waandishi wa habari tumeishi katika eneo lile zaidi ya miaka 50 lakini sasa hivi wanakuja kutuambia tuondoke kwenye eneo lile mara wanasema ni eneo la serikali,wakati mwingine wanasema ni eneo la TFS wanatutoa kinguvu kuna watu wamepotea wameacha watoto wakiwa peke yao hatujui walipo kwasababau ya ghasia hizo,

"Sasa leo(Jumamosi)tumekuja Dodoma tunataka kumuona Waziri Kuu atusaidie kilio chetu kifike kwa Rais mama yetu Dkt.Samia,tunaonewa hatuna nyumba wamebomoa,mazao wamechoma tuende wapi na sisi ni watanzania,"alisema Naoki.

Naye Eliha Lissu ni miongoni mwa wananchi waliofiki jijini hapa alisema kuwa lengo lao ni kuonana na Waziri Mkuu kwasababu Tanga hawajapewa ushirikiano wowote kutoka kwa viongozi wa mkoa wa Tanga akiwemo Mkuu wa Mkoa,Mbunge na Mkuu wa Wilaya.

Lissu amesema kuwa licha ya kupoteza makazi yao wananchi amedai kuwa watishiwa maisha endapo wataendelea kufuatilia haki zao au kutoa taarifa kwa vyombo vya habari .

"Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa mwaka jana Martin Shigella alitoa maelekezo kupitia Barua ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)kutoa tamko la kuwa wanachi tuendelee kuishi lakini baada ya yeye kuondoka ndipo tumeanza kuchomewa nyumba na kufukuzwa kwa nguvu bila maelewano,"alisema Lissu.

Halima Saidi alidai kuwa yeye ni mzaliwa wa kijiji cha Bondo na ana miaka 56  katika eneo hilo  hivyo ameishi katika eneo hilo kwa  zaidi ya miaka 56 sasa wamelazimika kulala porini bila makazi wala chakula huku wakiwa hawajui hatma ya maisha yao ni nini

"Watu tunapigwa hadi wajawazito wanajifungulia njiani hatuna amani kama tupo nchi za wenzetu huko lakini sasa hivi tunataona Bondo,lazima tumuone Waziri Mkuu atusaidie,sisi tunataka tu kusaidiwa tupate mahali pa kuishi na kuendelea na shughuli zetu za kilimo tunakimbia kimbia kama wakimbizi,"alisema Halima.


Mkuu wa Wilaya Kilindi,Hamis Mgandila  alipotafutwa kwa njia ya simu na waandishi wa habari alisema kuwa anyone hilo ni msitu wa hidadhi ambao upo toka miaka ya 60 ambapo wananchi walikuwa wamevamia eneo la hifadhi ya msitu ambao walitakiwa kutoka na walishaenda Mahakamani na walishindwa walikuwa wanatakiwa kutoka.

"Kwahiyo lilifanyika zoezi tu la kuwaondoa kwenye maeneo hayo Lakini mkuu wa Mkoa wa sasa Batilda Burian alitoa notisi ya siku 14 wakitakiwa kuondoka 
Kikubwa wanatikiwa watii sheria maana yake ni msitu wa hifadhi toka miaka ya 60,

"Na mnatakiwa mjue dunia sasa inakabiriana na mabadiliko ya tabia nchi kwahiyo kama tutaendelea kuathiri hivi vyanzo pamoja na mazingira tafsiri yake kama nchi tunaenda sehemu ambayo inawezekana ikawa ni mtihani yale maeneo ambayo yametengwa kama hifadhi hususani maeneo yale kwahiyo wao walitakiwa kutii sheria tu na kuondoka ,"alisema.

Aidha alieleza kuwa jambo hilo ni  la muda mrefu hata kamati za bunge zilishaagiza na zilishaazimia ,kamati ya mawaziri nane walishatoa maelekezo jambo hilo limekwenda mahakamani na mahakama imetoa majibu yeye haoni kama kuna shida wananchi hao kuondoka katika msitu huo.

Kuhusu suala la wananchi kulalamika kudai  wanaondolewa kinguvu kwa kupigwa hadi wajawazito kujifungua kabla ya muda ,Mkuu wa Wilaya hiyo alisema kama wanaweza kuchukua hatua basi wachukue hatua lakini jambo ambalo limetendeka halina shida.Huku akisema yeye siyo msemaji wa hilo yupo Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa ndiye anayetakiwa kujibu kuhusu hilo.

Kuhusu serikali kuwapeleka eneo lingine Mkuu wa Wilaya hiyo alijibu lilikuwa eneo la uvamizi adhani kama kunammiliki yoyote wa eneo lile kaondolewa hao watu wote ni watu ambao walivamia.
Na kama walivamia waende wapi Mkuu huyo wa Walaya alijibu walikotoka.

Naye Mbunge wa Jimbo hilo Omary Kigua alipotafutwa kwa njia ya simu na jopo la waandishi wa habari waliokuwa wanasikiliza maoni ya wananchi hao alisema kuwa ni kweli analijua jambo hilo  zaidi ya miaka mitatu iliyopita na alitaka waandishi waandike kama anavyoongea.

Kigua amesema Bondo ni hifadhi ya Serikali ipo kwenye kijiji cha Mswaki na Bondo ina GN yake mwaka 61 ni eneo la serikali kwa hao wananchi tena siyo kwa wananchi wa Kilindi hao ni wananchi waliotoka maeneo mengine walio wengi wametoa Manyara,Babati mwanzoni walikuwa wanalima mashamba waliambiwa na watu wa TFS ili eneo lina mita za mraba 11,000 wakaambiwa waachiwe 3,000 wao wakakataa wakaenda wakashitaki Mahakamani mpaka Mahakama kuu mara mbili wameshindwa kesi.

Ameendelea Mbunge wa Jimbo hilo walivyoshindwa kesi mwaka wa juzi wakapewa notisi ya kuondoka kwenye eneo la serikali hilo siyo eneo la wazi ni eneo la serikali lipo chini ya TFS na walivyopewa taarifa hawakuondoka.

"Mara ya mwisho kabla ya kuondolewa kwa nguvu Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt.Batilda Burian alienda na viongozi wote wa TFS,Mkuu wa Wilaya na viongozi wote kuwapa taarifa siku 14 waondoke kwenye hilo eneo ,wenye busara na hekima wakaondoka wapo wachache ambao hawakuondoka kwahiyo waliondolewa na serikali wala hawakuondolewa na mtu mwingine yoyote na waliondolewa kwasababu eneo hilo siyo la kwao eneo hilo kipande kiko kilindi lakini eneo hilo liko mpaka handeni,

"Kimsingi malalamiko yao hayana hoja kwasababu walikwishapewa taarifa waondoke ni eneo la hifadhi na mimi kama Mbunge na watetea wananchi wangu sana tu ila eneo hilo ndilo lilikuwa linatuletea mvua kwenye Tarafa ya Mswati,mimi nipo kifua mbele kuhakikisha eneo hilo haliharibiwi mazingira yake kwa maana hatuwezi tukalima kila sehemu kwahiyo lazima muwe na maeneo yahifadhi kwajili ya kuleta mvua lakini pia kuhifadhi mazingira kwahiyo hilo ni eneo halali la watu wa TFS la serikali.

Kigua amesema kuwa Waziri wa Maliasili analijua asilimia 100 ,Mkurugenzi wa TFS analijua hilo jambo Lakini yeye kama Mbunge wa Jimbo hilo na viongozi wote wa Wilaya na Mkoa wote wameridhia kwamba eneo hilo liwe hifadhi ya msitu.

Suala la wananchi kudai wameuziwa na Serikali ya Kijiji,Mbunge huyo alisema kuwa sheria ya kuuziwa hekari 100 haipo inatakiwa wakupe hekari 50 tu wananchi hao hata kama waliuziwa kihalali walidhulumiwa na aliyewauzia.

"Sina chakuwasaidia,mimi ni mwana mazingira na wala sina ugomvi nao ni wapiga kura wangu hao na kura zao nazitaka sana lakini ukipima kura zao na mazingira utaona mazingira yananafasi kubwa sana leo tupo kesho hatupo ,leo kilindi yote ukiifanya iwe jangwa mvua tutapata wapi lakini pia lile eneo ni la serikali kwahiyo mimi nikubali eneo la serikali liuzwe,"alihoji Mbunge huyo.

Kigua alisema kuwa chombo kinachoaminika ni Mahakama,kama walishindwa Mahakama kuu walipaswa waende Mahakama ya Rufaa na sijawaruhu wapigwe na kama wamepigwa na jeshi la polisi wanajua msemaji wa jeshi la polisi ni IGP kama ni TFS wawaulize wenye eneo lake siyo yeye.

"Ahaaa haaa!mimi niliwashauri tu jamani ee acheni hilo eneo,tena mwanzoni ndiye niliyewambia jamani kubalini hekari 3000 wakakataa na eneo hilo hilo kuna shule ya serikali na mimi Mbunge nimetoa mabati na simenti katika ile shule na bado wameambiwa ile shule itabakia pale watoto wao wataendelea kusoma.

Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt.Batilda Burian awali  alisema kuwa suala la misitu ni la  Wizara ndiyo wanafahamu yeye hajui na suala la wananchi 
kunyanyaswa na kupigwa alijibu kuwa hajui ndiyo kwanza amelisikia kwa mwandishi wa habari aliyepiga simu kutaka kujua zaidi juu ya mgogoro huo.

Dkt. Batilda  alikiri kufahamu mgogoro huo ambapo alisema ni kweli  eneo hilo  ni la TFS na waliwapa maelekezo Jeshi la wananchi kwajili ya mazoezi kwahiyo suala la jeshi kwenda kufanya hilo zoezi tunalijua.

"Hayo mengine yakuchomewa sijapata kuona wala kusikia najua heshima na nidhamu ya jeshi letu hawajawahi kufanya mambo ya uzembe yakifedhuri ndiyo maana hata wanapokwenda katika vikosi vya mazoezi huko Congo wanafanyakazi ya heshima na hawajawahi kulaumiwa kama majeshi mengine yanavyolaumiwa .

"Jeshi jina lake ni Jeshi la wananchi wapo kwajili ya kusimamia masuala mazima ya ulinzi wa wananchi walipokwenda kule ni kwenye zoezi na wananchi waliambiwa muda mrefu watoke mwezi mzima walipewa muda na walitoka bila kuguswa.Tuliwambia kuna maeneo yalikuwa yametengwa Kilindi na Handeni watumie taratibu wanazotumia wananchi wengine kupata maeneo .

"Haiwezekani mtu akaamua kutoka mkoa wowote au hata wilaya yoyote utoke Manyara uhamie kwenye msitu halafu uache tu ukae kila mtu atahamia kwenye msitu wake na Tanzania itakuwa tena haina msitu wafate sheria na taratibu za Serikali,mwananchi yoyote anayetaka afate taratibu,"alisema Mkuu wa mkoa huyo.

Amesema kilichofanyika ni walielezwa muda mrefu na kamati ya mawaziri ilitembelea Tanzania nzima na ikatoa ushauri kunamisitu ilikutwa na wananchi wakaachiwa lakini siyo msitu wa Bondo

GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.

GHARAMA YA KUPANDIKIZA MIMBA NI MILIONI 14 MUHIMBILI.

MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.

MOI Imefanikiwa Kuanzisha Huduma Zaidi ya 10 lkiwemo Upasuaji wa Ubongo Bila Kufungua Fuvu.

RIKA LINALOTAKA KUPANDIKIZWA MIMBA NI KUANZIA MIAKA 35 HADI 50.

RIKA LINALOTAKA KUPANDIKIZWA MIMBA NI KUANZIA MIAKA 35 HADI 50.

Vikundi 21 kunufaika na Mradi wa Tuinuke Pamoja Kukuza Usawa wa Kijinsia Kondoa, Chemba

Vikundi 21 kunufaika na Mradi wa Tuinuke Pamoja Kukuza Usawa wa Kijinsia Kondoa, Chemba

JAMII IMEHAMASISHWA KUZINGATIA MTINDO BORA WA MAISHA KWA KUFANYA MAZOEZI ILI KUJIEPUSHA NA MAGONJWA YA MOYO

JAMII IMEHAMASISHWA KUZINGATIA MTINDO BORA WA MAISHA KWA KUFANYA MAZOEZI ILI KUJIEPUSHA NA MAGONJWA YA MOYO