DKT.NCHIMBI AKEMEA KITENDO CHA MAKADA CCM KUTENGENEZA MATUKIO BINAFSI KWA KIVULI CHA CCM NA KUWALIPA POSHO WANACHAMA. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Siasa

DKT.NCHIMBI AKEMEA KITENDO CHA MAKADA CCM KUTENGENEZA MATUKIO BINAFSI KWA KIVULI CHA CCM NA KUWALIPA POSHO WANACHAMA.

Katika siku za hivi karibuni kumezuka utaratibu kwa baadhi ya makada wa CCM kutengeneza matukio ya kumbukizi za kuzaliwa,kumbukizi za ndoa na kuwaalika wanachama na kuwalipa posho.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
19 Feb 2025
DKT.NCHIMBI AKEMEA KITENDO CHA MAKADA CCM KUTENGENEZA MATUKIO BINAFSI KWA KIVULI CHA CCM NA KUWALIPA POSHO WANACHAMA.

Hayo yameelezwa na  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt Emmanuel Nchimbi leo February 19 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya Watendaji wa Kata na Makatibu Tawi wa Mkoa wa Dodoma .

Aidha ametoa Rai kwa Makada wanaofanya sherehe binafsi kwa kivuli cha chama na kuwataka kuacha Mara moja kwani ni kinyume cha utaratibu wa chama hicho.

"Niseme wazi  chama Cha Mapinduzi CCM kinamfumo wake wa kufuatilia kila kinachotokea  na kumbukumbu hizi tunazokusanya ndizo zitakazowaengua au kuwatoa kwenye kugombea, " Amesema Dkt

Aidha akielezea mafunzo hayo amesema
ni maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan lengo likiwa ni kuwa na watendaji  wanaotambua wajibu wao .

" Mafunzo haya yanakwenda kuwakumbusha majukumu yenu kama watendaji wa chama na jinsi gani tutashinda kwa kishindo uchaguzi mkubwa wa Rais, Wabunge na Madiwani, " Amesema

Na kuongeza " Hii iko wazi lengo kuu la chama chochote cha siasi ni kushika dola hivyo kwa upande wetu dola tumeshika kikubwa ni kushinda kwa kishindo kwani kushindwa kwa chama ni kunatokana na wanachama husika na kushinda kwa chama kunategemea wanachama hivyo tukawe waadilifu, " Amesema

Kwa upande wake  Katibu NEC Organization Issa Haji Gavu  amesema mafunzo hayo ni maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kusimamiwa na Katibu Mkuu Dkt  Nchimbi.

" Kwanini mafunzo haya kwa watendaji hawa ni kwasababu chama kipo  na kinaanzia kwenye ngazi ya Shina hadi Taifa hivyo niwaombe muwe wasikivu na kuzingatia mnavyoelekezwa, " Amesema Gavu.

Naye Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga amesema mafunzo hayo kwa watendaji wa Kata na Matawi yanakwenda kuwajenga kwani wapo nyuma ya muda na mafunzo haya yataleta muongozo .

Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.

Mavunde Agawa Kompyuta na Printa kwa shule zote za Sekondari za Jiji la Dodoma.

RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya  Migogoro ya Ardhi Nchini.

RAIS SAMIA Aagiza Mamlaka Za Serikali za Mitaa Kujiepusha Kuwa Vyanzo vya Migogoro ya Ardhi Nchini.

DAWASA Imeendelea na Utekelezaji wa Miradi Zaidi ya 25 Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 987.6.

DAWASA Imeendelea na Utekelezaji wa Miradi Zaidi ya 25 Yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 987.6.

JAJI WARIOBA: NAPONGEZA CCM KWA HATUA ZAKE DHIDI YA RUSHWA.

JAJI WARIOBA: NAPONGEZA CCM KWA HATUA ZAKE DHIDI YA RUSHWA.

WATENDAJI UBORESHAJI WA DAFTARI MOROGORO, TANGA WAHIMIZWA KUZINGATIA SHERIA.

WATENDAJI UBORESHAJI WA DAFTARI MOROGORO, TANGA WAHIMIZWA KUZINGATIA SHERIA.