MABADILIKO YA TABIA YA NCHI CHANZO CHA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA MAZAO | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kilimo

MABADILIKO YA TABIA YA NCHI CHANZO CHA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA MAZAO

Mabadiliko ya tabia ya nchi yanapelekea ongezeko la joto na kujaribu kupunguza maeneo na hali ya hewa ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mazao.

Moreen Rojas, Dodoma
By Moreen Rojas, Dodoma
07 Nov 2024
MABADILIKO YA TABIA YA NCHI CHANZO CHA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA MAZAO

Hayo yameelezwa na Dr.Sophia Kashenge Mkurugenzi wa uhaulishaji wa teknolojia na mahusiano katika taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kwenye mkutano ambao unawaunganisha wana sayansi wote katika mazao ya kilimo ulioandaliwa na Crop Science Association of Tanzania(CROSAT)uliofanyika tarehe 6 octoba jijini Dodoma.

Aidha amesema kuwa wakulima wameweza kupatiwa mbinu ya namna gani ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanaweza kuathiri uzalishaji wa mazao na kuweza kuandaliwa ili kumfikia mkulima kupitia vipeperushi mbalimbali,semina pamoja na vyombo vya habari kufikisha ujumbe Kwa wakulima

"Changamoto za kilimo ni nyingi na Sisi kama TARI kazi yetu kubwa ni kutafuta teknolojia mbalimbali na kuzipeleka kwa wakulima kwahiyo kama TARI tumeweza kubuni teknolojia nyingi zikiwemo mbegu mbalimbali zinazostahimili mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na teknolojia za uzalishaji ili kuwafikia wakulima hivyo lengo letu kubwa ni kufanya utafiti lakini kuhakikisha lakini kuhakikisha utafiti huo unaofanyika unawafikia wakulima"Amesema Kashenge

Aidha amesema mkutano huo umewakutanisha watu mbalimbali kuanzia wakulima mpka watu wa vyuo vikuu pamoja na taasisi mbalimbali lengo ni kujadili mambo yote yanayohusiana na uzalishaji wa mazao lakini hasa wakiangazia mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoendelea hivi sasa.

"Tumeona kumekuwa na mawasilisho mengi lakini mengi yamelenga katika kutengeneza suluhu katika mabadiliko ya tabia ya nchi na tumeona pia baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wameweza kuwasilisha mawasilisho yao lakini kimsingi ni mkutano ambao umeanza kufanyika ndani ya miaka ya hivi karibuni na huu ni mkutano wa kwanza wa kisayansi"

Aidha ameongeza kuwa ni mkutano ulioleta utatuzi ambapo changamoto kubwa iliyoletwa na wakulima ni changamoto ya Gugu Karoti ambapo ni changamoto kubwa hasa katika maeneo ya Arusha na Moshi na pia limesambaa katika maeneo mengi hivyo kupitia mkutano huu wanajikuta mambo muhimu yanaweza kuchangiwa na mwisho wa siku kupeleka maoni serikalini.

"Sisi kama TARI tumenufaika na mkutano huu haswa kuja kujifunza mambo mengi na haswa wafanyakazi wetu ambao wamekuja kutoa mawasilisho wamejifunza mambo mengi"


Kwa upande wake Prof.Kalunde Sibuga Rais wa chama Cha wataalam wa Sayansi ya mimea yaaani Crop Science Association of Tanzania (CROSAT) amesema wamekuwa wakipokea mada mbalimbali za mimea vipando,viatilifu,visumbufu vya mimea na njia ya kupambana na visumbufu hivyo na njia ambayo haitegemei tu madawa ya viwandani pamoja na kuzungunzia kilimo ikolojia,faida zinazotokana na kilimo ikolojia ili kuhakikisha wanazalisha chakula ambacho ni salama.

Naye Nuhu Aman kutoka taasisi ya kahawa Tanzania ambaye ni mshiriki wa mkutano  amesema mkutano huu umekuwa ni sehemu kubwa ya kujifunza mambo mengi ikiwemo namna bora ya kulima na aina za teknolojia zinazovumbuliwa kadri siku zinavyokwenda.

"Kupitia mkutano huu tumeweza kuona mawasilisho ya kisayansi kuelezea namna gani tunaweza tukatoka hatua moja kwenda nyingine na kuweza kuendeleza kilimo chenye tija na kipato kwa mkulima mdogo kulingana na namna bora ya kulima na aina mbalimbali za teknolojia ambazo zinakuja"Amesisitiza Nuhu.


Sanjari na hayo Jenipher Tairo ambaye ni Afisa mawasiliano msaidizi CROSAT amesema watu wanoweza kujiunga na taasisi hiyo ni wakulima,wanafunzi wa vyuo vikuu,maafisa kilimo pamoja na watu wenye makampuni mbalimbali ya kibinafsi yanayojihusisha na kilimo mazao,wadau wote wanaohusika na sekta ya kilimo mazao.

Aidha ameongeza kuwa kujiunga na CROSAT kuna faida nyingi kwa sababu ni jukwaa ambalo unapata nafasi ya kukutana na watu wanaofanya kitu ambacho unafanya hivyo ni sehemu nzuri ya kubadilishana uzoefu,hivyo anamwalika kila mtu ambae ni mdau wa kilimo mazao ambapo jinsi ya kujiunga ni www.crosat.or.tz

TANZANIA MWENYEJI WA JUKWAA LA TASNIA YA KUKU SADC.

TANZANIA MWENYEJI WA JUKWAA LA TASNIA YA KUKU SADC.

BASHE ALETA KICHEKO KWA WANANCHI WA LWINGA MKOA WA RUVUMA.

BASHE ALETA KICHEKO KWA WANANCHI WA LWINGA MKOA WA RUVUMA.

WAZIRI JAFO AHIMIZA WMA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA VIPIMO KWA JAMII

WAZIRI JAFO AHIMIZA WMA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA VIPIMO KWA JAMII

RC SENYAMULE:AIPONGEZA KAMPUNI YA PASS LEASING KWA KUWAFIKIA WAKULIMA

RC SENYAMULE:AIPONGEZA KAMPUNI YA PASS LEASING KWA KUWAFIKIA WAKULIMA