Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila ametoa rai kwa wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi siku ya Novemba 27,2024 kupiga kura na kuchagua viongozi kwani uchaguzi huo utakuwa na amani na utulivu na jeshi la polisi limejipanga vizuri kuhakikisha utulivu na amani vinapatikana wakati watu wa zoezi hilo.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Novemba 25,2024 mkuu huyo wa mkoa amesema hali ya usalama kwa mkoa ipo vizuri na yeyote atakae haribu hali hiyo hataachwa salama bali hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
"Niwatoe wasiwasi wananchi jitokezeni mkapige kura na mkimaliza nendeni kwenye majukumu yenu askari wapo kila sehemu tena wakutosha watalinda amani",Amesema.
Aidha ameongeza kuwa kuna uwepo wa 4R za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan zenye kuhimiza ustahimilivu unaongeza chachu kwa taifa hivyo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi itapelekea nchi kuvuka kihunzi kwenye maswala ya demokrasia
"Uchaguzi si kipimo cha demokrasia bali uchaguzi huo unapaswa kuwa huru na haki lakini unaoakisi zile 4R ambazo Rais Dkt Samia ameziasisi",Amesema.
Aidha amesema kuwa mkoa wa Dar es salaam unamitaa 564 hivyo wanatarajia kupata wenyeviti 564 na wajumbe wengi ambao wapo katika kila mitaa.
"Kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya viongozi walienguliwa kwenye mchakoto lakini kuna Vyama vingi sana vimeshiriki na vimesimamisha wagombea katika maeneo mbalimbali hivyo ni matumaini yetu wale wapenzi wa vyama vingi tarehe 27,watashiriki uchaguzi ili kuchagua viongozi wanaowataka",Amesema.
Sambamba na hayo akizungumzia maendeleo ya uokozi katika janga la kupotomoka kwa jengo la ghorafa tatu Kariakoo amesema zoezi bado linaendelea na hivi karibuni Waziri mkuu ataoa taarifa rasmi lakini pia atawajuza wafanyabiashara wa pembezoni watajuzwa lini watafungua biashara zao na pia atatoa taarifa za hatua zilizofikiwa ikiwemo ubomoaji wa jengo hili.
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.
SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA
RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO KWA WANANCHI WA SONGWE
UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.
THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.
ARUSHA NA KILIMANJARO KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA DESEMBA
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.