

Foundation For Disabilities Hope, taasisi isiyokuwa ya kiserikali, imepata ufadhili wa shilingi milioni 40 kwa ajili ya mradi wa kuwawezesha watu wenye ulemavu katika masuala ya uongozi na kukuza demokrasia.
Ufadhili huo umetolewa na shirika la Abilis Foundation yenye ofisi zake nchini Tanzania, mkoani Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Foundation For Disabilities Hope, Michael Salali, alisema mradi huo unalenga kuwafikia watu 300 wenye ulemavu katika wilaya ya Kondoa.
“Tunaimani mradi huu umekuja kwa wakati muafaka, hasa baada ya uchaguzi mdogo na kuelekea uchaguzi mkuu.
"Tunataka kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu kujitokeza kuchagua na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi bila kujihisi wanyonge,” alisema Salali.
Hata hivyo Tasisi hiyo imeishukuru Abilis Foundation kwa kufanikisha mradi huo muhimu.
Kwa upande wake Furaha William, Afisa Habari wa taasisi hiyo, alieleza kuwa mradi huo pia unalenga wanawake na wasichana kwa kuwajengea uwezo katika uongozi na ujasiriamali.
Alisisitiza kuwa jamii inapaswa kubadili mtazamo na kuwapa wanawake na watu wenye ulemavu nafasi za kutoa maamuzi.
“Sisi kama Foundation tunataka kuonyesha kuwa wanawake wanaweza kutoa maamuzi makubwa, kama Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye ni mfano mzuri wa uongozi bora,” alisema Furaha.
Aidha, alibainisha kuwa walichagua wilaya ya Kondoa kwa sababu imekuwa ikisahaulika katika miradi mingi ya maendeleo.
Mradi huu unatarajiwa kuwa chachu ya mabadiliko ya kijamii kwa kuimarisha ushiriki wa watu wenye ulemavu na wanawake katika uongozi.
WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WAASWA KUZINGATIA MADILI
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI
WAGOMBEA NAFASI YA NGAZI YA URAIS CCM KUTAMBULISHWA KWENYE MIAKA 48 YA CHAMA HICHO.
SERIKALI KUFANYA SENSA YA UZALISHAJI VIWANDA KWA MWAKA WA REJEA 2023.
AZANIA BENKI BUNGE BONANZA LAWALETA PAMOJA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA.
MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA KUKUTANA KATIKA BONANZA LA KUHAMASISHA MICHEZO NA UMUHIMU WA MAZOEZI.
MABADILIKO YA SERA YA ELIMU KUAKISI MABADILIKO YA KITAIFA NA KIMATAIFA.
RASMI UZINDUZI WA SERA YA ELIMU KUFANYIKA TAREHE 1 FEBRUARI 2025.
WASIRA: CHADEMA MSIJE NA AZIMIO LINALOKIUKA SHERIA ZA NCHI YETU.
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUHAKIKISHA KILA ENEO LINATAMBULIKA KWA ANWANI YA MAKAZI