Msemaji kutoka kampuni ya urekebishaji na utunzaji wa magari, THE WHEEL, Chris Mendoza, amesema uzinduzi wa teknolojia hiyo mpya utaleta mapinduzi makubwa katika sekta ya huduma za magari kwa mafundi.
Akizungumza Leo Novemba 30,2024 katika hafla ya uzinduzi huo, Mendoza alieleza kuwa teknolojia hiyo si tu itaokoa muda bali pia itaongeza usalama wa mafundi wanapofanya kazi zao.
Amesisitiza kuwa kupitia teknolojia hii, mafundi watakuwa na uwezo wa kugundua matatizo ya magari kwa haraka zaidi, jambo ambalo litapunguza muda wa matengenezo na kuongeza ufanisi wa kazi. "Hii ni teknolojia mpya ya namna ya utengenezaji wa magari, hivyo ni fursa kubwa kwa mafundi kujifunza na kuboresha maarifa yao," alisema Mendoza.Pia aliongeza kuwa teknolojia hiyo itahusisha vifaa vya kisasa vinavyotumia akili bandia (AI) na mifumo ya uchanganuzi wa data, jambo litakalorahisisha utambuzi wa hitilafu hata kabla ya kufanyika kwa ukaguzi wa kina wa gari. "Tunatarajia kuona mafundi wakifanya kazi kwa ufanisi mkubwa, wakipunguza makosa, na kuhakikisha magari yanarejeshwa kwa wateja katika hali bora zaidi," aliongeza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya The Wheel Amin Lakhani amesema wamefurahi kupanua huduma hadi Dodoma ambapo lengo ni kuboresha uzoefu wa Uendeshaji Kwa wateja wao.
Aidha Mkurugenzi huyo amesisitiza kuwa, Dodoma ina nafasi nzuri ya kuwekeza kutokana na kuwa mji mkuu na hivyo kuwashauri wawekezaji wengine kuwekeza zaidi katika mji huu na kueleza kuwa kuwepo kwa huduma bora za magari kutachangia katika kukuza uchumi wa mji na taifa kwa ujumla." Kampuni ya The Wheel inatarajia kuwa kituo hiki kitatoa ajira kwa vijana na kusaidia kuimarisha miundombinu ya usafiri katika mji wa Dodoma,kwa ujumla leo tunafurahi kufungua kituo cha kwanza hapa Dodoma ambapo itakuwa ni Cha saba kwa Tanzania,Mtanzamo wetu unahusu ubora,usalama na uamunifu huku tukihakikisha Kila safari inakuwa kadri ya maono yetu, "Amesisitiza.
KAMPUNI ya The Wheel imefungua kituo Cha utoaji huduma za urekebishaji wa haraka na utunzaji wa magari jijini Dodoma Ikiwa ni kituo cha saba Cha kutoa huduma nchini Tanzania.
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.
SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA
RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO KWA WANANCHI WA SONGWE
UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
ARUSHA NA KILIMANJARO KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA DESEMBA
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.
SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA