NAIBU waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko ameitaka Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi wa Usafiri majini Barani Afrika kushirikiana na kuungana ili kuimarisha usalama wa sekta ya usafirishaji majini ili kuchochea maendeleo ya Uchumi katika nchi husika.
NAIBU waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko ameitaka Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi wa Usafiri majini Barani Afrika kushirikiana na kuungana ili kuimarisha usalama wa sekta ya usafirishaji majini ili kuchochea maendeleo ya Uchumi katika nchi husika.
Wito huo umetewa leo Novemba 29, 2024 wakati akifungua Kongamano na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jumuiya ya Mamlaka za Usimamizi na Usafirishaji Majini Barani Afrika unaofanyika kwa siku tatu, Jijini Dar es Salaam wenye kauli mbiu isemayo 'kuimarisha Mustakabali wa sekta ya usafiri majini barani Afrika,ushirikiano katikà teknolojia na ubunifu ili kupunguza hewa ukaa kuimarisha usalama wa mazingira na mazingira ya usafiri kwa mustakabali endelevu'.
Aidha Dkt. Biteko amewashauri washiriki kutumia mkutano huo kama fursa ya kubuni na kupanga mikakati mipya ya kuelekea katika mafanikio kupitia sekta hiyo ambapo amesisitiza kuwa ushirikiano miongoni mwa washiriki na kujadiliana juu ya kuwezesha masuala mbalimbali na sekta ya usafirishaji ndio suluhisho la changamoto mbalimbali zilizopo.
“Kila mmoja wetu atumie fursa ya mkutano huu kujiwekea malengo yatakayo tuwezesha kufikia azma ya kuboresha usalama na kuimarisha sekta ya usafirishaji wa majini” amesema Dkt. Biteko.
Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema miongoni masuala yanayohitaji kutiliwa mkazo ni pamoja na suala la raslimali watu hususan vijana ambao watachagiza uendelevu na ukuaji wa sekta ya usafiri na usalama wa usafirishaji wa majini.
Profesa Mbarawa amesema Tanzania kwa upande wake imekuwa mstari wa mbele ikitekeleza maazimio ya uboreshaji wa sekta hiyo ikiwa ni pamoja na miradi mikubwa inayolenga pamoja na mambo mengine lakini kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa.
Ameongeza kuwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam na ujenzi wa Reli ya Umeme kutoka Dar es Salaam - Morogoro hadi Dodoma mbali na kuongeza ufanisi katika usafirishaji, pia inapunguza uchafuzi wa mazingira.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Masuala ya Baharini (IMO), Arsenio Dominguez ameipongeza Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa Kongamano na Mkutano huo kwani nchi inaoonesha utayari wake katika uboreshaji wa sekta ya usafirishaji na usalama wa majini.
Dominguez amesema IMO itaendelea kuwezesha vikao hivyo vya kimataifa ili kujenga na kuimarisha ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama ili kukabiliana na changamoto za bahari katika nchi husika.
Amesema IMO ina program nyingi zinazohusu hifadhi ya mazingira na uwezeshaji kuelekea usawa wa kijinsia ambapo lengo ni kuwawezesha wanawake kwani wako nyuma katika masuala ya usafirishaji na usalama majini.
Awali akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam na hivyo kupunguza msongamano katika upakiaji na upakuaji wa mizigo Bandarini hapo.
“Tunaomba ufikishe salam hizo kwa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mwambie tunamshukuru kwa huduma za uboreshaji wa Bandari yetu ya Dar es Salaam sasa hivi hatuna msongamano wakati wa kupakia au kupakua mizigo Bandarini, amesema Mpogolo.
Naye, Mkurugezi mkuu wa Shirika la uwakala wa meli nchini TASAC, Mohamed Salum ameaema jumla ya nchi 45 zimeshiriki katika mkutano huo hivyo wanategemea baada ya mkutano huo utaenda kufungua fursa nyingi katika usafiri wa bahari lakini pia mkutano kuja na suluhisho la kupunguza uchafunzi wa mazingira ya bahari.
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.
SERIKALI YA SAMIA KUZALISHA AJIRA MPYA MILIONI 1.2 KILA MWAKA
RAIS SAMIA APELEKA KICHEKO KWA WANANCHI WA SONGWE
UZINDUZI WA TEKNOLOJIA MPYA YA UREKEBISHAJI NA UTUNZAJI WA MAGARI KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI.
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.
THE WHEEL YALETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA HUDUMA ZA MAGARI NCHINI.
ARUSHA NA KILIMANJARO KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA DESEMBA
SERIKALI YATAKA MAFANIKIO SEKTA YA MAJI YALINDWE
WATU WENYE ULEMAVU WAMEPATA UFADHILI KWA AJILI YA KUWAWEZESHA KATIKA MASWALA YA UONGOZI NA KUKUZA DEMOKRASIA.