TAASISI ZA UMMA ZAHIMIZWA KUTENGA ASILIMIA 30 YA BAJETI YA MANUNUZI KWA AJILI YA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM. | The Dodoma Post
The Dodoma Post Biashara

TAASISI ZA UMMA ZAHIMIZWA KUTENGA ASILIMIA 30 YA BAJETI YA MANUNUZI KWA AJILI YA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM.

Serikali imeendelea kuhimiza Taasisi za umma kutenga asilimia 30 ya bajeti ya manunuzi kwa ajili ya wanawake na makundi maalum.

moreen Rojas, Dodoma
By moreen Rojas, Dodoma
12 Nov 2024
TAASISI ZA UMMA ZAHIMIZWA KUTENGA ASILIMIA 30 YA BAJETI YA MANUNUZI KWA AJILI YA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM.

Hayo yameelezwa na Felister Mdemu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na makundi Maalum wakati wa ufunguzi wa mafunzo yanayohusu ushiriki wa wanawake na makundi maalum katika manunuzi ya Umma Tarehe 12 Novemba 2024 jijini Dodoma yaliyoandaliwa na chama Cha Wanawake Wafanyabiashara  Tanzania(TWCC).

Aidha amesema kuwa Kwa kutenga asilimia hizo kutawawezesha kunufaika na tenda zinazotolewa na Serikali pamoja na Taasisi za umma na kusisitiza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mipango ya Serikali kuhakikisha wanawake na vijana wanaongeza ushiriki na kunufaika na fursa hii ya asilimia 30% ya bajeti ya manunuzi ya umma inayotengwa kwa ajili yao kila mwaka.

Aidha ameongeza kuwa Wizara yake imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika kuwezesha wanawake kiuchumi nchini na TWCC ni mdau mmojawapo katika eneo la kiuchumi.

"Sote tunatambua kuwa ushiriki wa wanawake na vijana katika ununuzi wa umma bado unakabiliwa na changamoto kubwa, changamoto hizo mara nyingi hutokana na ukosefu wa utaalamu,taarifa zisizotosha kuhusu michakato ya zabuni,gharama ya upatikanaji wa mitaji pamoja na wajasiriamali wengi wadogo kuendelea kutokuwa na vigezo vya kukopesheka"

"Kwa wajasiriamali wote wanawake na vijana hapa leo ninawahimiza kutumia fursa hii adhimu,kuuliza maswali,kushirikiana na wakufunzi na kushirikiana na wenzao kwa kujenga mtandao wa kufanya kazi kwa umoja,hii ni fursa yao ya kupata zana,ujasiri na msaada wanaouhitaji ili kushiriki kikamilifu na kufanikiwa kupata zabuni,mikataba ya sekta ya umma na ya kibinafsi,maarifa wanayotapata leo si kwa ajili ya biashara zao tu bali kwa jamii nzima na maendeleo ya taifa letu"

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TWCC Bi.Mwajuma Hamza ametoa shukrani za dhati kwa Mhe Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaunga mkono wanawake na vijana kupitia juhudi za kuwawezesha kiuchumi na kuwafungulia milango ya fursa ndani na nje ya nchi,vilevile amewapongeza washiriki waliochangamkia fursa hii na kuwataka kuzingatia elimu waliyopewa ili iweze kuleta manufaa kwao binafsi na kwa taifa kwa ujumla.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema kikubwa kwao ni taarifa ya namna gani ya kufanya manunuzi kwani wengi hawana taarifa za kutosha kwani wafanyabiashara wengi hawajui tenda ni nini na wanafanya vipi manunuzi hivyo elimu ya kutosha inapaswa kutolewa kwa wajasiriamali wadogowadogo.

"Tunaomba Serikali itupatie mikopo na kuangalia namna ya kutuwezesha Kwa namna yoyote ile Kwa sababu unaweza ukapata tenda lakini mtaji ukawa ni mdogo hivyo naiomba Serikali ituangalie kwa jicho la tatu huku wakizingatia kutupati taarifa Kwa wakati lakini hata ukipata taarifa na hiyo tenda bila mtaji wa kutosha huwezi kufanya kitu chochote maana suala la fedha linakwisha kwa namna nyingine"Amesisitiza Joyce Said mshiriki wa mafunzo hayo

Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania(TWCC) ni chama kikuu kilichoanzishwa mwaka 2005 Kwa lengo kuu la kukuza uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake Tanzania ambapo chama hiki kina zaidi ya wanachama 10,000 kutoka katika matawi 27 ya mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

NIC YAZINDUA KAMPENI YA NIC KITAA ILI KUTOA ELIMU YA BIMA KWA WANANCHI.

NIC YAZINDUA KAMPENI YA NIC KITAA ILI KUTOA ELIMU YA BIMA KWA WANANCHI.

TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini

TRA yaahidi kuwa na usawa kwa wafanyabiashara Nchini

VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI

VIONGOZI SOKO LA MACHINGA DODOMA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI

BRELA YAWATAKA WASANIFU MAJENGO NA WAJASIRIAMALI KUTUMIA VIZURI BUNIFU ZAO.

BRELA YAWATAKA WASANIFU MAJENGO NA WAJASIRIAMALI KUTUMIA VIZURI BUNIFU ZAO.

MCHENGERWA AZINDUA MFUMO WA KADI JANJA ZA MWENDOKASI AWATAKA DART NA UDART KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAGARI.

MCHENGERWA AZINDUA MFUMO WA KADI JANJA ZA MWENDOKASI AWATAKA DART NA UDART KUTATUA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAGARI.