SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima | The Dodoma Post
The Dodoma Post Kijamii

SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Alhaj Mustafa Rajabu Shaban ametunukiwa Udaktari wa heshima(PhD)huku akiahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha heshima hiyo inaleta manufaa kwa jamii hususani kwa watu walioko kwenye mazingira magumu.

Moreen Rojas
By Moreen Rojas
15 Nov 2024
SHEKHE wa mkoa wa Dodoma atunukiwa Udaktari wa Heshima

Aidha Shekhe Mustafa ni mmoja kati ya watunukiwa nane wa PhD ambao wamedhaminiwa  na Chuo cha Outreach Care International kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornerstone  International  College cha USA, Lucent University cha uengeleza  na HHWB College - USA


Akizungumza kwenye halfa ya kumpongeza hivi karibuni Jijini hapa amesema tunu hiyo sio sifa ya kujiona kuwa fahari mbele ya jamii bali itamchochea katika kuongeza uwajibikaji kwa kuitumikia jamii ikiwa ni pamoja na kuendelea kueneza mafundisho ya wema, heshima na kumtumikia Mungu kwa njia sahihi.

"Katika maisha yangu ya dini, nimedhamiria kila wakati kuwa mfano mzuri wa maadili, amani, na mshikamano,nimejizatiti katika kueneza ujumbe wa upendo, ushirikiano, na mshikamano kwa ajili ya amani ya nchi yetu,na hili ndilo lengo langu kila wakati kwa sababu tumetumwa kuitumikia jamii na kuongeza juhudi zaidi tofauti na tulivyofanya mwanzo, "amesema

Shekhe Mustafa pia amesema, "Nashukuru  kwa fursa hii ya kipekee, ambapo leo hii nimepata heshima ya kutunukiwa udaktari wa heshima, ni heshima kubwa ambayo siwezi kuikwepa bila kumshukuru Mungu na kuwashukuru watu wote walioshirikiana nami katika safari yangu ya maisha, " amesema na kuongeza;

"Nawashukuru sana viongozi wa dini, viongozi wa Serikali, na wadau wengine wote ambao wamekuwa sehemu ya mafanikio yangu na mimi kuweza kuleta mchango wangu katika jamii yetu ya Dodoma na Tanzania kwa ujumla, " ameeleza

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaji Shekimweri ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo ameeleza kuwa tunu hiyo ina mafundisho katika jamii kwamba penye nia na malengo, juhudi na dhamira ya dhati,  Mungu hufanikisha.

Amesema kutunukiwa udaktari wa heshima  siyo tu heshima  binafsi, bali ni heshima ya  jamii na wote waliokuwa na imani na juhudi katika kuleta mabadiliko chanya.

Shekimweri pia ametumia nafasi hiyo kumuomba Shekhe huyo kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kusaidia watu, kuhimiza mshikamano na amani, na kuhakikisha kwamba maadili  yanaendelea kuwa mwanga kwa jamii .

Naye Mhadhiri wa masomo na msimamizi kwa njia ya mtandao  Dkt .Kharid Salaa ametumia nafasi hiyo kuwashauri  Wahitimu wa  elimu ya vyuo vikuu mara wanapohitimu kutekeleza majukumu yao ya kazi na uongozi kwa ushirikiana na jamii inayowazunguka ikiwemo kuwafumdisha ujuzi walioupata ili kujenga Taifa.

Dkt Brigit Terry Beemudu  mmoja wa wahitimu Hao amesema mefanya kazi zaidi ya 30 za kujitolea bila kulipwa, kwa umri huo ni sawa na binti ambaye angekuwa na familia yake

Katika kazi ya kujitolea niliweza kuriski familia yangu kwa sababu nilitumia muda mwingi kuihudumia jamii na kuiacha familia yangu

Mfano nilipotoka kufuatilia suala LA matumizi ya vifanyio watu walikuwa wanapokezana lakin lengo lilikuwa ni kuibua na kuelimisha jamii juu ya ukimwi.

BALOZI NCHIMBI KUONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO.

BALOZI NCHIMBI KUONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KIBIKI LEO.

PLAY MATTERS KUFIKIA SHULE 31 KIBONDO KUTOA ELIMU KWA WATOTO KWA NJIA YA MICHEZO.O.

PLAY MATTERS KUFIKIA SHULE 31 KIBONDO KUTOA ELIMU KWA WATOTO KWA NJIA YA MICHEZO.O.

DCEA YABAINI WAFANYABIASHARA WA SHISHA WANAOCHANGANYA BIDHAA HIYO NA DAWA ZA KULEVYA.

DCEA YABAINI WAFANYABIASHARA WA SHISHA WANAOCHANGANYA BIDHAA HIYO NA DAWA ZA KULEVYA.

AWESO,BASHUNGWA WAJADILI MIKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KATIKA JIJI LA TANGA.

AWESO,BASHUNGWA WAJADILI MIKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KATIKA JIJI LA TANGA.

Vyuo Vikuu Dar vyatambulisha tamasha la UNIFEST 255.

Vyuo Vikuu Dar vyatambulisha tamasha la UNIFEST 255.